Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Habari

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mhandisi Hagai Mziray wa Mzinga Corporation kuhusu ramani ya jengo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara zinazojengwa na Kampuni ya Mzinga Corporation inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania leo jijini Dodoma.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na Watendaji wa Kampuni ya Ujenzi ya Mzinga Corporation alipokuwa akifanya ukaguzi katika wa Ofisi zinazojengwa na Kampuni hiyo leo Ihumwa jijini Dodoma. Wizara zinazojengwa na Kampuni hiyo ni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michez, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Wizara ya Madini na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Lekumock Ponja akisikiliza maelezo kutoka kwa Fundi Sanifu wa Mzinga Corporation, Keneth Wambua kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi leo jijini Dodoma.

Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Lekumock Ponja akitazama ujenzi wa jengo la Ofisi ya wizara hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi leo jijini Dodoma.

Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Lekumock Ponja (kushoto) akitazama mchoro wa jengo la Ofisi ya wizara hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za wizara hiyo leo Ihumwa jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Katibu Muhtasi wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sana na Michezo, Bibi. Munieshi Mushi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara hiyo, Bi. Lorietha Laurence na Mhandisi Hagai Mziray wa Mzinga Corporation.

Baadhi ya mafundi wa Kampuni ya ujenzi ya Mzinga Corporation wakiendelea na majukumu yao ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kama walivyokutwa leo jijini Dodoma.

Muonekano wa nje wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zinazojengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama