Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasilisha azimio la Bunge kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) leo Bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mara baada ya kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akitoa maelezo kuhusu matumizi ya silaha za jadi hapa nchini na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia uzagaaji wa silaha hizo.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Mhandisi Gerson Lwenge akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi katika Wilaya ya Ngara wanapata huduma za maji.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia injinia Stella Manyanya akitoa ufafanuzi kuhusu jinsi Serikali ilivyofanikiwa katika mpango wa elimu bure hapa nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Tate Ole Nasha akizungumzia mkakati wa Serikali kuhakikisha kuwa Maafisa ugani katika maeneo yote hapa nchini wanatekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuwahudumia wananchi.
(Picha na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma) P

36 thoughts on “Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama