Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisisitiza kuhusu umuhimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu na kuepuka vitendo vyote vya kuwabugudhi wafanyabiashara wakati wa kutekleza jukumu la kukusanya kodi katika maeneo yote nchini wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu leo Bungeni  Jijijni Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job  Ndugai akisisitiza jambo wakati akijibu miongozo ya wabunge  leo Bungeni  Jijini Dodoma  mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt.  Mwigulu  Nchemba akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 leo Bungeni Jijini Dodoma.

 Sehemu ya wageni waliofika bungeni  wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi  Isack Kamwelwe akitoa maelezo kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kufikisha huduma za maji kwa wananchi kote nchini.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu taratibu za matibabu hasa kuhusu kitendo cha baadhi ya viongozi kuonyesha mfano katika kutoa chanjo cha wasichana wenye umri wa miaka kuanzia 14 ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

Mbunge wa viti maalum (CCM) Mhe. Amina Mollel akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanajengewa mazingira rafiki yatakayowawezesha kushiriki katika ujenzi wa uchumi.

( Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

173 thoughts on “Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama