Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika Picha Bungeni leo

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao  cha tano cha  mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Kapt Mstaafu George Mkuchika  akilieleza Bunge  kuwa Serikali imeshatoa kibali cha kuajiri watumishi wapya 15000 ili kuziba pengo lilisababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi  wa umma waliobainika kughushi vyeti leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile akielezea  mpango mkakati uliowekwa na Serikali ili  kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na  watoto ikiwemo kupitia kamati za ulinzi zilizowekwa  wakati wa kikao cha tano mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akieleza faida za kupatikana kwa Sera mpya ya Maendeleo ya Michezo leo Bungeni  Jijini Dodoma,  ambapo amesema uratibu wa rasimu kamili ya sera hiyo umefikia hatua za mwisho na Wizara yake itakamilisha zoezi hilo ndaniya muda mfupi ujao.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Omary Mgumba akieleza tozo mbalimbali zilizotolewa na Serikali katika zao la kahawa  ambapo imesaidia kuimarisha bei ya kahawa nchini wakati wa kikao cha tano mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu akieleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha huduma ya umeme nchini wakati wa kikao cha tano mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea Jijini Dodoma.

5 thoughts on “Matukio katika Picha Bungeni leo

 • August 11, 2020 at 1:43 pm
  Permalink

  Everyone loves what you guys tend to be up too.
  This sort of clever work and reporting! Keep up the amazing works guys I’ve incorporated you guys to
  my personal blogroll.

  Reply
 • August 12, 2020 at 1:45 am
  Permalink

  Hi my family member! I wish to say that this post is amazing,
  nice written and come with approximately all vital infos.
  I’d like to peer extra posts like this .
  adreamoftrains best web hosting sites

  Reply
 • August 24, 2020 at 10:35 am
  Permalink

  Hey There. I found your blog using msn. This is a very well written article.
  I’ll be sure to bookmark it and return to read more of your useful information. Thanks for the post.

  I’ll certainly return.

  Reply
 • August 31, 2020 at 4:12 am
  Permalink

  I think the admin of this web page is genuinely working hard for his site, for the reason that here every
  data is quality based information.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama