Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika picha Bungeni Leo

Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Tulia Ackson akitambulisha wageni wa jukwaa la Spika wakati wa kikao cha thelathini na tano cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe.Mboni Mhita akitoa shukurani mbele ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania toka achaguliwe kuongoza umoja huo ivi karibuni nchini Afrika ya kusini ambapo atatumikia kwa muda wa miaka mitatu.

 

Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mhe.Stephen Maselle akitoa shukurani mbele ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania toka achaguliwe kuongoza Bunge hilo  ivi karibuni nchini Afrika ya kusini.

Wanafunzi wa Sekondari ya Huruma ya Jijini Dodoma(kushoto) na Wanachuo wa Chuo cha Diplomasia(kulia) wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Augustine Mahiga akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Augustine Mahiga na Naibu wake Mhe.Dkt.Suzan Kolimba wakipitia hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kabla ya kuwasilisha leo Jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum Mhe.fatma Toufiq(CCM) akiuliza swali kutaka  kujua  mpango wa Serikali kudhibiti hali ya wanafunzi kupewa ujauzito na  waendesha bodaboda leo Jijini Dodoma.

125 thoughts on “Matukio katika picha Bungeni Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama