Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Aprili 23, 2019

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza umuhimu wa waandishi wa Habari kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kulinda tunu za Taifa leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimisha mjadala wa hoja zilizotolewa kwa wabunge wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wake Mhe. Juliana Shonza mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo leo bungeni Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifurahia jambo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Susan Mlawi wakifuatilia majadiliano ndani ya ukumbi wa ubunge leo kabla ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2019/2020.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa Wizara mara baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kushughulikia makosa ya jinai ikiwemo kufanya uchunguzi dhidi tuhuma husika na kubaini ukweli.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisisitiza kuhusu utaratibu unaotumiwa na Shirika la Fedha Duniani kutoa taarifa ya hali ya uchumi kwa nchi wananchama Leo Bungeni Jijini Dodoma.

Mmoja wa wasanii akimpongeza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo leo Jijini Dodoma.(Picha zote na Frank  Mvungi- MAELEZO, Dodoma)

80 thoughts on “Matukio Katika Picha Bungeni Aprili 23, 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama