Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bunge Leo

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akihitimisha hoja baada ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Fedha wa mwaka 2018 baada ya kupitishwa na Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasilisha tamko kuhusu mashindano ya pili ya riadha ya wanawake nchini yatakoyofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 24 na 25/11/2018 leo Bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Huruma Mkuchika(kushoto) wakati wa kikao cha tisa Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Hanang’I, Mhe. Mary Nagu(kushoto) wakati wa kikao cha tisa Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akiteta jambo na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko(kulia) wakati wa kikao cha tisa cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akifuatilia hotuba ya hitimisho la hoja ya muswada wa sheria ya huduma za fedha ya mwaka 2018 wakati wa kikao cha tisa Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuf Singo (katikati) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) na Mbunge wa Same Magharibi, Mhe. Dkt. David Mathayo David.

Baadhi ya wageni wa Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakitambulishwa Bungeni leo jijni Dodoma. Wageni hao ni wanafamilia ya Clouds Media ambao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya Tamasha la Fiesta.(Na Mpiga Picha Wetu)

One thought on “Matukio Katika Picha Bunge Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama