Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Marekani Yaipatia Tanzania Dola Mil. 225 za Maendeleo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (kushoto) akisaini mkataba wa Makubaliano (Strategic Assistance Agreement ) na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas (katikati) kuhusu utoaji wa fedha  dola za kimarekani milioni 224 zaidi ya Shilingi bilioni 499 tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani  nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson akishuhudia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (kushoto) akibadilishana mkataba ya makubaliano (Strategic Assistance Agreement) na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas mara baada ya tukio hilo la mkataba wa makubaliano katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama