Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Marais Wastaafu Waungana na Rais Dk. John Pombe Magufuli Katika Mazishi ya Dada Yake

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Share

Marais Wastaafu waliopokelewa kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza ni Mzee Ali Hassan Mwinyi, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mzee Benjamin William Mkapa  huku wakiongozana na wake zao kama wanavyoonekana pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mh. Raila Odinga

Kama anavyoonekana Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza kwa Ndege ya Shirika la ATCL Boeing 787-8 Dreamliner jijini Mwanza.

 

Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza mara baada ya kwasili uwanjani hapo leo akielekea Chato.

Mzee Benjamini William Mkapa akiwasili uwanjani hapo kwa ndege ya ATCL tayari kuelekea wilayani Chato kwa mazishi ya Marehemu Monica Joseph Magufuli.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akiongozana na Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini wakati wakielekea Chato.

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Share

Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mh. Raila Odinga akipokelewa wilayani Chato mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Chato kwa ajili ya kuhudhuria mazisho ya Bi. Monica Joseph Magufuli dada wa Rais Magufuli.

Marais Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na wake zao kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza ni Mzee Ali Hassan Mwinyi, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mzee Benjamin William pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Marais Wastaafu wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kushuka kwenye Ndege Boeing 787-8 Dreamliner katika uwanja wa Ndege wa Mwanza ni Mzee Ali Hassan Mwinyi, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mzee Benjamin William pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Magari mbalimbali yaliyoandaliwa kuwasafirisha viongozi hao kwenye wilayani chato yakiwa katika uwanja wa ndege wa mwanza.

Viongozi mbalimbali wakipokelewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella wakati wakishuka kwenye ndege ya ATCL katika uwanja wa Ndege wa Mwanza leo.

Viongozi mbalimbali wakiwemo Marais Wastaafu pamoja na viongozi kutoka nje ya nchi wameendelea kupokelewa kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza wakielekea Mkoani Geita wilaya ya Chato kwa ajili ya kushiriki katika mazishi ya Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli Marehemu Monica Jospeh Magufuli yanayotarajiwa kufanyika leo wilayani huo.

Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza kwa Ndege ya Shirika la ATCL Boeing 787-8 Dreamliner jijini Mwanza.

2 thoughts on “Marais Wastaafu Waungana na Rais Dk. John Pombe Magufuli Katika Mazishi ya Dada Yake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama