Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali kuanzisha maaba ya vinasaba vya wanyama

Jengo la mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kaskazini-Arusha

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini – Arusha,  ipo mbioni kuanzisha Maabara maalum Vinasaba vya wanyama ambayo itasaidia kutambua  asili ya mnyama ikiwemo wanyama waliopo ama waliokufa.
Akizungumza wakati wa ziara maalum ya Maafisa Uhusiano waliotembelea Kanda hiyo leo, Meneja Kanda ya Kaskazini Christopher Anyango abainisha kuwa kwa sasa wapo katika ukarabati wa jengo ambalo Maabara hiyo itakuwepo. Awali ujenzi wa jengo hilo ulisimama baada ya ufadhili wake kukoma na hivyo kuilazimu Mamlaka  kufanya ukarabati ili kujipatia sehemu ya kufanyia kazi.
“Maabara ya vinasaba vya wanyama ni muhimu sana. ukanda huu kutokana na kuwa na wanyama wengi na pia eneo la Kanda ya Kaskazini kuwa na watalii wengi ambao wanakuja kuona wanyama . Kwa sasa utaratibu unaendelea wa Kumalizia jengo hili na baadaye vitendea kazi kuwekwa “ameeleza Anyango.

Meneja Kanda ya Kaskazini Christopher Anyango(mwenye suti) akiwatembeza maofisa habari wa wizara na taasisi wa wizaravya afya wakati walipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa kampeni ya “Tumeboresha Sekta ya Afya”ambayo imeanza kwa mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Kilimanjaro.

Anyango ameongeza kuwa suala la kuwatunza wanyama ili waendelee kuwepo, Ni suala la msingi na Maabara itakapokamilika hakuna sampuli zitakazosafirishwa nje ya  Kanda ya Kaskazini kwa uchunguzi.
“Pale  hitaji litakapokuwapo kwa ajili ya uchunguzi wa wanyama hawa, baasi Kazi hii itafanyika hapa hapa Arusha.” Alisema Anyango.
Aidha, ametaja faida ambazo zitapatikana kwa Nchi ni pamoja na uwepo wa data zao kwa wanyama hao ikiwemo wanyama wanaolindwa Kimataifa kama Kifaru, tembo na wanyama wengine wengi ambao wapo hatarini kutoweka.
Maabara hii inatarajiwa kuwa ya kwanza Nchini na itakuwa ndio maabara Bora kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Maabara hiyo itaweza kufanya uchunguzi kwa wanyama wote wakiwemo walio hai na waliokufa.
Aidha, wamemshukuru Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Rais Dk Joseph Pombe Magufuli kwa kutenga  na kuridhia kiasi  cha bajeti ya Shilingi  Milioni 950 ya kwa ajili ya kumalizia  jengo hilo.

17 thoughts on “Mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali kuanzisha maaba ya vinasaba vya wanyama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama