Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mama Samia Ahimiza Jamii Kuhusu Utunzaji wa Mazingira

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua kuelekea Baharini katika maeneo ya Ilala Bungoni na Temeke kwa Aziz Ally Jijini Dar es Salaam leo. Mifereji hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo lengo ni kunusuru hali ya mafuriko katika maeneo hayo. Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando.

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa mafundi wa wanaojenga mfereji wa maji taka eneo la Ilala Bungoni alipotembelea mradi huo leo Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya mfereji unaojengwa katika eneo la Ilala Bungoni kwa ajili ya kupeleka maji hadi katika bonde la mto msimbazi ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo mafuriko.

Sehemu ya mfereji unaojengwa katika eneo la Temeke kwa Aziz Ally kwa ajili ya kusafirisha maji ya ikiwa ni njia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo mafuriko.

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiulizia jambo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa mfereji wa maji katika eneo la Ilala Bungoni leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba.

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiulizia jambo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa mfereji wa maji kuelekea baharini katika eneo la Temeke kwa Aziz Ally leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

82 thoughts on “Mama Samia Ahimiza Jamii Kuhusu Utunzaji wa Mazingira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama