Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mama Salma Kikwete Ashiriki Katika Uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili Nchini Kenya.

Balozi wa Kiswahili Afrika Mama Salma Kikwete akiongea wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili nchini Kenya katika Jengo la Kenya Institute of Curriculum Development, Nairobi, Kenya ambapo ameahidi kuitumia kwamanufaa ya Tanzania, Kenya, East Afrika, Afrika na Duniani kwa Ujumla.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili nchini Kenya katika Jengo la Kenya Institute of Curriculum Development, Nairobi, Kenya.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Kenya Dkt. Fred Matiang’i, akiongea wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili nchini Kenya katika Jengo la Kenya Institute of Curriculum Development, Nairobi, Kenya.

Balozi wa Kiswahili Afrika Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania, Kenya, Dkt. Pindi Chana (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili leo nchini Kenya. (Na: Mpiga Picha Wetu)

83 thoughts on “Mama Salma Kikwete Ashiriki Katika Uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili Nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama