Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Afanya Ukaguzi Mradi Uboreshaji Kingo za Bahari

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari ambao mradi unatekelezwa katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuoni hapo yenye urefu takribani mita 500. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira a Muungano January Makamba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi unatekelezwa katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) yenye urefu takribani mita 500. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira a Muungano January Makamba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano January Makamba akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) yenye urefu takribani mita 500 leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akielezea jambo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi ambao unatekelezwa katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) yenye urefu takribani mita 500.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari kutoka kwa mmoja wa wakandarasi wa mradi huo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa Kuimarisha Kingo za Bahari unatekelezwa katika kingo za Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) Kigamboni yenye urefu wa mita 500, Sea View yenye urefu wa mita 900, Pangani Tanga na Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipita juu ya Kingo ya Bahari iliyojengwa kupitia mradi wa uimarishaji wa Kingo za Bahari alipotembelea Fukwe ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo. Fukwe hiyo imefanyiwa maboresho ambapo kingo yake imejengewa njia ya wapita kwa miguu na sehemu za kupumzikia.

Sehemu ya Kingo iliyojengwa katika fukwe ya bahari ya hindi eneo la Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Siasa wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kigamboni alipokutana nao wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi unaotekelezwa katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) yenye urefu takribani mita 500. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Kate Mfutakamba. (Picha na Frank Shija – MAELEZO)

40 thoughts on “Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Afanya Ukaguzi Mradi Uboreshaji Kingo za Bahari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama