Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Azindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Kuzindua Mpango Mkakati Jumuishi wa kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Selemani Jaffo na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kuzindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

Baadhi ya Washiriki wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya kuzindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Septemba. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango(kushoto kwake) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakionyesha vitabu vya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katia Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe uliofanywa na Waziri Mkuu, kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama