Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Atoa Zawadi Mashindano ya Kusoma Qur-an Tukufu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakr Zubeir bin Ally (kulia) na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikima Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo , katika Mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mlezi wa Taasisi ya Al- Hikima Foundation, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 18 ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.

Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwanza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

30 thoughts on “Majaliwa Atoa Zawadi Mashindano ya Kusoma Qur-an Tukufu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama