Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Atembelea Gereza la Kwitanga Mkoani Kigoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mchikichi ikiwa ni ishara ya kuzindua mpango wa kupanua mashamba ya michikichi katika Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine ya kukamua mafuta ya mawese wakati alipotembelea Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma ambalo ni maarufu kwa kilimo cha michikichi, Februari 17, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua matrekta mawili aina ya Ursus yenye thamani ya shilingi milioni 145 yatakayosaidia kuinua kilimo cha michikichi katika Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma Februari 17, 2019.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha Trekta aina ya Ursus wakati alipozindua matrekta mawili yatakayosaidia kuinua kilimo cha michikichi katika Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019.

99 thoughts on “Majaliwa Atembelea Gereza la Kwitanga Mkoani Kigoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama