Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Ataka Waliopewa Uraia Kuheshimu Sheria

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihotubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Veta Jimbo la  Ulyankulu wilayani Kaliua Mkoani Tabora leo August 11.2017, ambapo amewataka wananchi waliopewa uraia kuheshimu sheria za nchi vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa CUF Jimbo la Kaliua ,Magdalena Sakaya. Leo Agosti 11.2017,Waziri Mkuu yupo wilayani Kaliua kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Tabora.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mwamnange kilichopo Wilaya ya Kaliua  leo  Agosti 11 2017. Wananchi hao walisimamisha msafara wake ili kumuomba serekali iwasaidie kupata  Umeme. Waziri Mkuu yupo Mkoani Tabora kukagua shughuli za maendeleo.

(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama