Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini Kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji kuuga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijijini Dar es salam, Julai 4, 2018.

Wapambe wa Bunge wakiwa wameubeba mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stehen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza Katika tukio la kuuaga mwiili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai wakisikiliza salamu mbalimbali za waombolezaji kabla ya kuaga mwiili wa mbunge wa Korogwe Vijijini , Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson , Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi, John Kijazi na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia wakati alipowaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

52 thoughts on “Majaliwa Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama