Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Akutana na Spika wa Bunge la Rwanda Donatile Mukabalisa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge la Rwanda, Mheshimiwa Donatile Mukabalisa kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Juni 11.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Rwanda waje wawekeze katika sekta mbalimbali na kwamba Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Juni 11, 2019) alipokutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Rwanda, Donatille Mukabalisa, Ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge la Rwanda, Mheshimiwa Donatile Mukabalisa, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Juni 11.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Amesema Serikali ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka katika nchi hiyo ili waje kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, kilimo, madini na utalii.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Tanzania na Rwanda ni nchi zenye uhusiano mzuri, hivyo amemwakikishia Spika Donatille kwamba Serikali itauimarisha uhusiano huo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao utarajiwa kusaidia katika usafirishaji wa mizigo kwenda hadi nchini Rwanda.

Naye, Spika Donatille ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa kwa Serikali ya Rwanda, hivyo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza.

Spika huyo amesema ushirikiano wa Tanzania na Rwanda ni muhimu katika uchumi kwa kuwa wanatumia bandari ya Dar es Salaam katika kusafirisha asilimia kubwa ya mizigo yao.

Amesema wananchi nao wanatakiwa wawe na ushirikiano katika nyanja mbalimbali kama za kibiashara. Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania wakawekeze nchini Rwanda.

6 thoughts on “Majaliwa Akutana na Spika wa Bunge la Rwanda Donatile Mukabalisa

 • August 10, 2020 at 3:56 am
  Permalink

  Howdy, I do believe your web site may be having web browser compatibility problems.
  When I take a look at your blog in Safari, it looks fine
  however, when opening in I.E., it has some overlapping issues.
  I just wanted to provide you with a quick heads up!
  Besides that, wonderful site!

  Reply
 • August 25, 2020 at 4:22 am
  Permalink

  Wow, wonderful weblog layout! How lengthy have you been blogging for?
  you make running a blog look easy. The whole look
  of your site is fantastic, let alone the content!
  3gqLYTc cheap flights

  Reply
 • August 26, 2020 at 2:36 am
  Permalink

  Pretty! This was an extremely wonderful post. Thanks for supplying this info.
  34pIoq5 cheap flights

  Reply
 • August 26, 2020 at 8:53 am
  Permalink

  Hurrah, that’s what I was seeking for, what a stuff! present here at this webpage,
  thanks admin of this website.

  Reply
 • August 31, 2020 at 3:46 am
  Permalink

  I would like to thank you for the efforts you have put in penning this website.

  I really hope to view the same high-grade blog posts
  by you later on as well. In truth, your creative writing abilities has encouraged me to get my own website now ­čśë

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev e┼čyas─▒ depolama