Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Aanza Ziara ya Mkoani Mara

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kuanza ziara mkoani humo Januari 15, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima,

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi waliofiika kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kumlaki baada ya kuwasili mjini Musoma kuanza ziara ya Mkoa wa Mara Januari 15, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya Rirandi ya asili ya kabila la Wakurya baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kuanza ziara ya mkoa wa Mara Januari 15, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua majengo ya Shule ya Secondari ya Ufundi Musoma akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 15, 2017.Serikali imetoa shillingi bilioni 1.28 kwa ajilli ya ukarabati huo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Samweli Kiboyi. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Mutta Venance.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya bweni la Shaban Robert wakati alipokagua ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 15, 2017. Serikali imetoa zaidi ya shilling bilion 1.28 ili kugharimia ukarabati huo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwangwa mjini Musoma akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 15, 2017. Kulia wake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 

54 thoughts on “Majaliwa Aanza Ziara ya Mkoani Mara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama