Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Magonjwa ya Moyo Huua Watu Milioni 17 Duniani – Dk. Sanga

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Lugendo akimpima shinikizo la damu (BP) Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa Leyla Faiz wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo na kutoa dawa bila malipo kwa kushirikiana na makampuni yanayotengeneza dawa za binadamu na Shirikisho la Magonjwa yasiyo kuwa ya Kuambukiza (TANCDA).

Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Louiza Shem akitoa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya moyo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Taasisi hiyo. Pamoja na kutoa elimu ya afya bora Taasisi hiyo imetoa huduma ya upimaji afya bila malipo na kutoa dawa bila malipo kwa kushirikiana na makampuni yanayotengeneza dawa za binadamu na Shirikisho la Magonjwa yasiyo kuwa ya Kuambukiza (TANCDA).

Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule akimpima sukari Charlote Guzuye mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.

Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lucy Nyawike akimpima shinikizo la damu (BP) Mwandishi wa Habari wa kituo cha Televisheni cha Clouds Rachel Chizoza wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aloyce Mohamed akimkabidhi dawa za ugonjwa wa moyo Abdala Shomvi mkazi wa Mkuranga Mkoani Pwani wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.

Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lucia Kabeya akimpima msukumo wa damu (BP) Subir wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.

7 Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hania Bwahama akimpima sukari Shabani Juma wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni ya dawa na chama ilitoa upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.

Madaktari wakitoa huduma ya ushauri kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Wananchi wakisubiri kupata huduma ya upimaji magonjwa ya moyo bure wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam. (Picha na: Paschal Dotto)

149 thoughts on “Magonjwa ya Moyo Huua Watu Milioni 17 Duniani – Dk. Sanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama