Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maambukizi ya Ukimwi Yapungua Hadi Asilimia 4.7

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi. (Picha na: Frank Shija)

Na: Emmanuel Ghula -NBS

KIWANGO cha maambukizi ya UKIMWI nchini kimepungua kutoka asilimia 5.1 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 4.7 mwaka 2016/2017.

Akizindua matokeo ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa Mwaka 2016/2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na janga la UKIMWI.

Amesema kwa mujibu wa utafiti huu wa mwaka 2016/17, inakadiriwa kuwa watanzania wapatao million 1.4 wanaishi na virusi vya UKIMWI. Alifafanua kuwa utafiti huo unaonesha kuwa kiwango cha maambukizi kwa wanawake ni asilimia 6.5 na wanaume ni asilimia 3.5.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa salamu za Ofisi yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAID) Dkt. Leonard Maboko akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.

Mh. Samia Suluhu amesisitiza kuwa kupungua kwa kiwango cha maambukizi hakumaniishi kuwa UKIMWI umeisha bali ni matokeo ya jitihada zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo wananchi katika kujilinda dhidi ya maambukizi mapya.

“Utafiti huu tunaouzindua leo umeonyesha kupungua kwa kasi ya maambukizi ya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 4.7 kwa mwaka 2016/2017. Hii inatokana na juhudi za pamoja kati ya Serikali, wananchi na wadau mbalimbali waliojikita katika kutoa elimu na huduma za masuala ya UKIMWI,” amesema Mh. Samia Suluhu.

Mh. Samia Suluhu ametoa wito kwa wananchi na wadau wengine kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kukabiliana na maambukizi mapya pamoja na kuchangia kwa hiari Mfuko wa Taifa wa UKIMWI ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora zinazohusu UKIMWI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu Jenista Mhagama (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAID) Dkt. Leonard Maboko wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kutoka katika baadhi ya mabanda aliyoyatembelea wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.

Mapema akitoa maelezo kuhusu utafiti huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa alisema kuwa huo ni utafiti wa nne kufanyika hapa nchini, ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 2003/04 ambao ulionesha kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 7.0  na kufuatiwa na tafiti nyingine za miaka ya 2007/08 na 2011/12 iliyoonesha maabukizi ya asilimia 5.1.

Alieleza kuwa utafiti wa 2016/17 umekuwa wa kipekee kwani unatoa makadirio ya kiwango cha maambukizi ya VVU kwa watu wa rika zote  ikiwa ni pamoja na maambukizi mapya ya VVU, kiasi cha VVU mwilini kwa wanaoishi na VVU, na kiwango cha kufubazwa kwa VVU mwilini kwa wanaotumia dawa za kufubaza VVU.

Aidha, utafiti huo unatoa kiwango cha maambukizi ya Homa ya Ini  na taarifa za upatikanaji wa huduma na matibabu kwa wanaoishi na VVU pamoja na ushauri nasaha, upimaji wa VVU na utoaji wa majibu, na kukusanya taarifa za kaya na taarifa binafsi za wanakaya.

Amesema utafiti huu ulihusisha kaya 16,198 na kujumuisha wanakaya wote waliokuwa kwenye kaya wakilishi zilizochaguliwa na umegharimu kiasi cha Shillingi 7.4 bilioni ambazo zimetolewa na Serikali ya Marekani chini ya Mfuko wa Rais
wa Dharura wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief – PEPFAR).

Baadhi ya wananchi wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akifurahi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu Jenista Mhagama,(kushoto) Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAID) Dkt. Leonard Maboko(kulia) mara baada ya kuzindua rasmi Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi leo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu ramani ya maeneo yaliyofanyiwa utafiti toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa mara baada ya kuzindua Matokeo ya Awali ya Utafiti wa Viashria na Matokeo ya Ukimwi leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu Jenista Mhagama na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAID) Dkt. Leonard Maboko (kulia).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mara baada ya kumalizika kwa shere wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Matokeo ya Awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi. (Picha na: Frank Shija)

Aidha, amesema mikoa ambayo kiwango cha maambukizi ya VVU ni zaidi ya asilimia 10 ni Iringa yenye maambukizi ya asilimia 11.3 na Njombe yenye asilimia 11.4 huku mikoa yote ya Tanzania Zanzibar ikiwa na maambukizi ya ukimwi ni chini ya asilimia 1.

Katika maelezo yake hayo, Dkt. Chuwa ameonya baadhi ya watu wanaopotosha takwimu rasmi za serikali na kueleza kuwa jambo hilo halikubaliki.

Alibainisha kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu haimzuii mtu kufanya tafiti kwani serikali inatambua kuwa tafiiti ni suala muhimu lakini katika kufanya hivyo lazima mtafiti afuate taratibu zilizowekwa.

Ametoa wito kwa serikali hususani wizara ya afya kutumia matokeo ya utafiti yaliyozindualiwa katika kupanga mipango ya sekta ya afya.

 

21 thoughts on “Maambukizi ya Ukimwi Yapungua Hadi Asilimia 4.7

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama