Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maafisa Utamaduni Jitokezeni kwa Wingi Kushiriki kikao Kazi – Susan Mlawi

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini kitakachofanyika tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo.Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Bw.Bonoface Kadili, na Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis Songoro.

Na Shamimu Nyaki –WHUSM.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi ametoa wito kwa Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri nchini kushiriki kwa wingi katika kikao kazi cha sekta hiyo kitakachofanyika  kuanzi tarehe 27 na 28 Februari 2019 Jijini Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma Bibi. Susan Mlawi ameeleza kuwa kikao hicho ni cha 11 kufanyika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Umoja Upendo na Kazi :Asili ya Utamaduni Wetu”  lengo ikiwa ni kuendeleza Sekta ya Utamaduni hapa nchini.

“Lengo la kikao kazi hichi ni kuweka mikakati ya pamoja katika kutekeleza Sera ya Utamaduni kwa ngazi ya Mikoa na Halmashauri pamoja na kuhamasisha ukuzaji na matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili ambayo ndio lugha inayotambulisha nchi yetu”. Alisema Bibi.Susan.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Bonoface Kadili akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi.Susan Mlawi (Katikati) azungumze na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini kitakachofanyika tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis Songoro.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (Mwenye blauzi nyeupe ) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini kitakachofanyika tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo.Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Bw.Bonoface Kadili, na Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis Songoro.

Ameongeza kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao kazi hicho anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe huku kikifungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jaffo.

Aidha Bibi. Susan amezitaja mada zitakazowasilishwa  katika kikao kazi hicho ambazo ni Ubidhaishaji wa Lugha ya Kiswahili,Utendaji kazi Kimuundo baina ya Maafisa Utamaduni wa Wizara Mikoa na Halmashauri,Uhuishaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni,Fursa za Utalii wa Kiutamaduni nchini.

Mada nyingine ni Ufahamu Kuhusu Haki Miliki na Hakishiriki za Wasanii,Fursa ya Soko kwa Bidhaa za Utamaduni pamoja na Mada itakayohusu Umuhimu wa Sekta ya Filamu katika kuimarisha Asili na Utamaduni wetu.

78 thoughts on “Maafisa Utamaduni Jitokezeni kwa Wingi Kushiriki kikao Kazi – Susan Mlawi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama