Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Uongozi wa New Habari inayomiliki magazeti ya Mtanzania, The African, Rai na Dimba Jijini Dar Es Salaam Jana alipowatembelea na kusikiliza changamoto zinazowakabili

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari Bw. Absalom kibanda wakati alipotembelea ofisi za New Habari na kusikiliza changamoto za kihabari za kampuni hiyo Jijini Dar Es Salaam

Na Grace Semfuko-MAELEZO

Msemaji  Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewatakaMaafisa Habari Nchini kufanya kazi zao kwa kufuata sheria yaHuduma za Habari ya mwaka 2016 ambayo inawapa fursaWaandishi wa Habari kupata,kuhariri na kurusha habari kwawananchi ili waweze kuelewa maendeleo ya nchi yao.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti JijiniDar Es Salaam Ijumaa Agosti 24, 2018 alipotembelea Kampuniya Magazeti ya New Habari na Shirika la Habarilinalounganisha Redio zenye Maudhui ya kijamii la TADIO ambao walimweleza Msemaji Mkuu wa Serikali kuhusiana.

 nachangamoto za kupata habari wanazofanyiwa na baadhi yaMaafisa Habari wa Taasisi  mbalimbali za Serikali Nchini.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiangalia baadhi ya magazeti ya kila siku katika ofisi za New Habari, Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Patrick Kipangula.

“Ni kweli wapo baadhi ya Maafisa Habari ambaowanakwamisha juhudi za waandishi kupata Habari,Idara yaHabari MAELEZO tumeliona hilo na tulishaanza mkakati wakuhakikisha kila taasisi inatoa habari ili wananchi waelewemaendeleo ya maeneo yao na taasisi hizo, tumekaa na MaafisaHabari mara kadhaa na tumewapa mafunzo na sasa changamotohiyo imepungua kwa kiasi kikubwa” alisema Dkt Abbasi.

Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba 5 Mwaka 2016 naKusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DktJohn Pombe Magufuli Novemba 16 mwaka huo huo wa 2016,pamoja na mambo mengine, inalenga kulinda maslahi yawaandishi wa habari,kulinda kazi zao pamoja na kuboreshaTaaluma hiyo ili iweze kuheshimika kama taaluma ilivyo kwazingine.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza katika kikao cha Watendaji Wakuu wa Taasisi inayoshughulika ma usimamizi wa maudhui kwenye radio za kijamii TADIO alipowatembelea katika Ofisi zao zilizopo kwenye jengo la ODL ndani ya chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) Jijini Dar Es Salaam Jana, Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Patrick Kipangula.

Aidha Dkt. Abbasi  amezungumzia mkakati wa kuanzishwa kwamfuko wa taaluma ya habari ili kuwawezesha waandishikumudu kufanya kazi za utafiti wa habari na vipindi mbalimbalivya kijamii badala ya kutegemea ruzuku za mashirika ambazopia huja kwa masharti ambayo mengi yanaweza kuwaingizahatiani.

Aidha Dkt. Abbasi pia amewakumbusha Waandishi wa Habarinchini kujiunga na vyuo mbalimbali ili kujiendeleza kitaalumana hatimaye waweze kuendana na kanuni ya kuwa na diploma itakayoanza kutumika mwishoni mwa mwaka 2021.

“Kanuni ya kumtaka mwanahabari awe na diploma kwenda juukatika fani ya habari itaanza kutumika mwaka 2021, tumetoamuda wa kutosha kabisa kwa waandishi kujiendeleza,kamahukufanya hivyo sheria haitakuruhusu kupata ithibati yakuendelea na majukumu ya kazi za Habari,” alisisitiza Dkt. Abbasi.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Patrick Kipangula (Wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi inayoshughulika na maudhui ya radio za kijamii TADIO kwenye nje ya Ofisi hizo Jijini Dar Es Salaam

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-MAELEZO ambayepia anashughulikia Usajili wa Magazeti Bw. Patrick Kipangulaamesema Sheria mpya ya Habari inalenga kuimarisha kazi zaWaandishi ili waweze kuheshimika na sio adhabu kama wengiwanavyoitafsiri na kuongeza kuwa Sheria hiyo imeweka bayananamna ambavyo Waandishi wa Habari watakavyonufaika nayo.

Amesema lengo ni kuwafanya waandishi wa Habari kufanyakazi zao kwa weledi mkubwa na kuhoji kuwa ni “kwa ninitaaluma zingine ikiwemo ya Sheria,Udaktari na nyinginezoziheshimike na sio kwa taaluma ya Habari? Ni lazima tuifanyetaaluma hii iheshimike” Alisema Kipangula.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda ameipongeza MAELEZO kwamageuzi makubwa katika kuisemea Serikali na kuongeza kuwaSheria ya Huduma za Habari imekuwa ni chachu kubwa yaWaandishi wengi wa Habari kuamua kwenda kuongeza elimu nakwamba wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu yaTano ya kuimarisha taaluma hiyo nchini kwa kuwaruhusuWafanyakazi wao kujiendeleza kimasomo.

Kibanda pamoja na mambo mengine alizungumzia changamotoya upatikanaji wa matangazo ya Serikali ambayo kwa kiasikikubwa alidai yamewaathiri kiuchumi ambapo Dkt Abbasalitumia ziara hiyo kufafanua kuwa unaandaliwa utaratibu mpyawa kuhakikisha matangazo ya taasisi za Serikali yanatolewa kwaufanisi.

“Matangazo ya taasisi za Serikali yalikuwa yakitolewa kiholelatu na yalikuwa yakiisababishia Serikali madenimakubwa,ukiangalia mfumo wa utoaji wa matangazo yenyeweutashangaa,mtu anakutana na kiongozi barabarani anamwambiaatoe tangazo na analitoa, hii ilikuwa changamoto kubwa kwasababu baadhi ya matangazo hayo hayakuwa kwenye Bajeti nahivyo kutengeneza madeni yasiyolipika,” alisema Dkt. Abbasi.

Ziara ya Dkt. Abbasi kwenye taasisi hizo za Habari  ilikuwa niya kujifunza na kutoa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tanowa kushirikiana na vyombo vya Habari katika kusimamiataaluma na kutangaza maendeleo ya nchi.

56 thoughts on “Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama