Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maafisa Habari Watakiwa Kuwa na Mawasiliano ya Kimkakati

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda akisisitiza jambo kwa Mwakililishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo wakati wa ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa Mtwara leo kuona utendaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja na changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua hali itakayoimarisha Mawasiliano Serikali kwa umma katika mkoa huo.

 

Mwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Afisa Mipango Mji Bi. Mariam Kimolo wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo hivi karibuni.

Frank Mvungi- MAELEZO

Maafisa Habari Katika Mkoa wa Mtwara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.

Akizungumza na Ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini  (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO uliomtembelea ofisini kwake , Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Alfred Luanda amesema kuwa jukumu la Maafisa Habari ni kuhakikisha kuwa masiliano kati ya Serikali na wananchi yanakuwa yakimkakati  na yanayoendana na kasi ya Serikali katika kuwahudumia wananchi.

“ Baadhi ya  Maafisa  Habari wanajiweka nyuma na kusahau kuwa wanalo jukumu kubwa la kuuhabarisha umma kuhusu miradi ya maendeleo inayoteklezwa katika maeneo yao hasa kwenye Mikoa na Halmashauri” Alisisitiza Luanda

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Bw. Omari Kipanga (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo hivi karibuni

Akifafanua amesema kuwa umuhimu wa Afisa habari unatokana na namna anavyotekeleza majukumu yake  kwa weledi hasa katika suala la mawasiliano ya kimkakati.

Aidha,  alipongeza kazi zinazofanywa na Idara ya Habari na chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.

Kwa upande wake muwakilishi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo amesema kuwa kila Afisa Habari ana jukumu la kuisemea Serikali katika Mkoa au Halmashauri ili kuwapa wananchi fursa ya kuelewa mikakati ya na miradi ya maendeleo inayoteklezwa katika maeneo yao na kuachana na kasumba ya kufanya kazi kwa mazoea.

Afisa Habari wa Mkoa wa Mtwara Bw. Evaristi Masuha akisisitiza jambo kwa Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo hivi karibuni

Naye Kiongozi wa ujumbe huo Bi. Gaudensia Simwanza amesema kuwa kuna haja kwa maafisa habari kupanua wigo wa utoaji wa taarifa za miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Aliongeza kuwa Lengo la chama cha maafisa habari na mawasiliano Serikalini ni kuwajengea uwezo katika kuisemea Serikali.

Ziara ya ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) katika Mkoa wa Mtwara , Lindi na Ruvuma inalenga kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma kwa kuweka mikakati ya pamoja kati ya ujumbe huo Maafisa Habari, na Viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wakurugenzi wa Halmashuri za Mikoa hiyo.

56 thoughts on “Maafisa Habari Watakiwa Kuwa na Mawasiliano ya Kimkakati

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama