Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Akutana kwa Mazungumzo na Balozi wa Finland Nchini

<

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Adolf Mkenda akimkaribisha Wizarani Balozi wa Finland nchini, Mhe. Pekka Hukka alipofika kwa ajili ya kujitambulisha kwake kama Katibu Mkuu mpya na kuzungumzia jinsi ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Finland. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 09 Novemba,  2017.
Prof. Mkenda akimweleza jambo Balozi Hukka wakati wa mazungumzo yao. Pamoja na mambo mengine wlizungumzia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya elimu, biashara na uwekezaji ambapo Prof. Mkenda alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi Hukka kwa msaada unaotolewa na Serikali yake kwa Taasisi ya Uongozi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvatory Mbilinyi kwa pamoja na Bi. Tunsume Mwangolombe wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Balozi Hukka (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea

 

 

>

30 thoughts on “Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Akutana kwa Mazungumzo na Balozi wa Finland Nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama