Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Katibu Mkuu Dkt. Ulisubisya Akutana na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya (aliyesimama), akiongea na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Makao Makuu na Kanda ya Mashariki, mara baada ya kuwatembelea leo. Wa pili kutoka kushoto ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice M.S. Mafumiko pamoja na Wakurugenzi wa Idara.

 

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice M.S. Mafumiko, akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya (aliyevaa miwani) kuongea na watumishi mara baada ya Katibu Mkuu kutembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo.

Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Makao Makuu na Kanda ya Mashariki, wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) alipotembelea Ofisi za Mamlaka kuonana na watumishi hao.

 

Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bw. Aidan Maganigani (kushoto), akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya watumishi mara baada ya Katibu Mkuu kumaliza kuongea na watumishi.

86 thoughts on “Katibu Mkuu Dkt. Ulisubisya Akutana na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama