Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kamishna Uhamiaji Zanzibar afanya ziara Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja

Afisa Uhamiaji Wilaya ya Kusini Mkaguzi Msaidizi  wa Uhamiaji, Kheri Shabani akitoa mkono wa salamu kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wakati alipowasili kwenye Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo,   tarehe 21 – 22 Novemba, 2017. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akitia saini kitabu cha wageni, mara tu alipowasili Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani humo, Leo tarehe 22 Novemba, 2017. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Mkemimi Mohamed Mhina.

 
 Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Khamis Ali Juma akitoa
maoni juu ya changamoto wanazokabiliana nazo katika eneo la uendeshaji wa
mashtaka ya Kiuhamiaji, wakati wa kikao cha pamoja cha Wafanyakazi wa Mkoa wa Kusini
Unguja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wakati alipofanya
ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 – 22 Novemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Akijibu hoja mbali mbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 – 22 Novemba, 2017.  Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdullah Mbarouk Ramsa.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akielezea jinsi Idara ya Uhamiaji inavyopiga hatua katika kutatua changamoto ya Makaazi ya Askari wake katika Wilaya zote Unguja na Pemba. Aliayasema hayo wakati akikagua nyumba za Watumishi wa Uhamiaji iliyopo Makunduchi, Wilaya ya Kusini, wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika tarehe 21 – 22 Novemba, 2017.Imetolewa Na: Kitengo Cha Uhusiano, Ofisi Kuu Ya Uhamiaji Zanzibar

 

73 thoughts on “Kamishna Uhamiaji Zanzibar afanya ziara Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama