Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Yavutiwa na Utendaji wa Idara ya Maafa ya Tanzania Bara

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akifafanua jambo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ya Zanzibar walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam, wengine ni waratibu wa maafa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

Na.Mwandishi Maalum. Dar es Salaam 

Kamisheni ya Kukabiliana na maafa Zanzibar imevutiwa na shughuli za kuratibu maafa nchini zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Idara ya Kuratibu maafa ikiwa ni pamoja na kuratibu Afya moja ambapo katika Dhana ya Afya Moja, sekta ya   afya ya binadamu, wanyama (pori na wafugwao) na mazingira, zinakuwa na mawasiliano ya karibu kiutendaji na kupanga  mikakati ya pamoja katika kujiandaa na milipuko ya magonjwa na kukabiliana nayo endapo itatokea.

Akiongea wakati wa  ziara ya Kubadilishana Uzoefu na Idara ya Kuratibu Maafa na Ofisi ya Waziri Mkuu,Jijini Dar es salaam leo tarehe 15 Novemba 2017, Mkurugenzi Mtendaji Kamishseni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Shaban Mohamedi amebainisha kuwa kamisheni yake imevutiwa na jinsi idara ya maafa inavyoweza  kuimarisha juhudi na ushirikiano wa sekta mbalimbali katika maandalizi ya kuzuia,kujiandaa na kukabili  magonjwa ambukizi kwa kujumuisha sekta zote muhimu.

“Tutaupitia mpango mkakati wa Afya moja  ili nasisi tuanze juhudi za kuratibu Afya moja  kwani Kamisheni inajukumu lakukabiliana na Maafa hivyo tutachukua juhudi za kuhakikisha na sisi Zanzibar tunashirikiana na wadau husika ili tuweze kutumia rasilimali ndogotulizonazo kuweza kukabili magonjwa yatokayo kwa  wanyama kwenda kwa binadamu yanayoiathiri jamii ya Zanzibar” alisisitiza Khatibu.

Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya (Kulia), Mkurugenzi mtendaji Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Operesheni na Huduma za Binadamu Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya Kamisheni hiyo na Idara ya maafa walipofanya ziara ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.

Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Edgar Senga akiwasilisha mada ya majukumu ya idara hiyo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ya Zanzibar walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Operesheni na Huduma za Binadamu Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib akiwasilisha mada ya majukumu ya Kamisheni hiyo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya , alifafanua kuwa suala la Afya moja linaratibiwa na ofisi yake kupitia Dawati maalum kutokana na kuwa magonjwa ya mlipuko ni masuala mtambuka na yanahitaji rasilimali watu na fedha nyingi hivyo kwa uratibu wa pamoja inasaidia kuhakikisha sekta zote zinashirikiana kukabiliana na athari za magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

“Umuhimu huu wa Afya moja unatokana na ukweli kwamba magonjwa na athari nyingine za binadamu kwa kiasi cha asilimia 60 hadi 80 huusisha wanyama. Kwa kufanya hivi ufanisi huongezeka kwani mchanganyiko wa Wataalamu, wakifanya kazi kwa pamoja na ushirikianao mkubwa, huchukua muda mfupi, na  matumizi ya raslimali chache kwa pamoja huleta matokeo mazuri zaidi” Alisema Msuya.

Mwaka 2013, aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya nne, ya Jamhuriya MuunganowaTanzania, Dk. Ghalib Bilal alizindua mtandao wa afya moja jijini Arusha. Kufuatia uzinduzi huo, mwaka 2015 wadau kutoka sekta mbalimbali walikaa na kutengeneza mpango mkakati wa afya wa miaka mitano (2015 – 2020). Mpango huo umeainisha masuala yahusuyo afya moja, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa utaratibu wa kuratibu shughuli zote za afya moja katika idara ya kuratibu maafa katika ofisi ya waziri mkuu.

7 thoughts on “Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Yavutiwa na Utendaji wa Idara ya Maafa ya Tanzania Bara

 • August 11, 2020 at 5:00 am
  Permalink

  For newest news you have to go to see internet and on world-wide-web I
  found this site as a most excellent website for most recent updates.

  adreamoftrains web hosting service

  Reply
 • August 14, 2020 at 1:39 pm
  Permalink

  Simply wish to say your article is as astounding.
  The clarity in your post is simply nice and i could assume you’re an expert on this subject.
  Well with your permission allow me to grab your RSS feed to keep
  updated with forthcoming post. Thanks a million and
  please carry on the rewarding work.

  Reply
 • August 26, 2020 at 12:26 pm
  Permalink

  It’s not my first time to pay a visit this website, i am visiting this web site dailly and take nice data from here daily.

  34pIoq5 cheap flights

  Reply
 • August 27, 2020 at 12:14 am
  Permalink

  Right now it looks like BlogEngine is the best blogging platform out
  there right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

  Reply
 • September 5, 2020 at 3:34 pm
  Permalink

  Excellent items from you, man. I have have in mind your stuff prior to and you’re simply too fantastic.
  I really like what you’ve acquired right here, really like
  what you’re stating and the way in which during which you say it.
  You’re making it enjoyable and you continue to care for to
  stay it smart. I cant wait to learn far more from you. That is really
  a wonderful site.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama