Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kalemani, Mgalu Waongoza Kikao cha Majadiliano Mradi Wa Lng

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiongoza kikao kujadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG), kilichofanyika Aprili 30 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri Subira Mgalu.

Na Veronica Simba – Dodoma

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu wameongoza kikao kilichojadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG).

Kikao hicho kilifanyika Aprili 30 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kushirikisha Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na wataalamu kutoka wizarani.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu (kushoto), wakiongoza kikao kujadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG), kilichofanyika Aprili 30 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Wengine pichani ni Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi, wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, wajumbe kutoka TPD, EWURA na PURA.

Kikao kikiendelea

Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, wakiwa katika kikao hicho.

Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, wakiwa katika kikao hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama