Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

JPM, Museveni Wawataka Wananchi Kutumia Fursa Bomba la Mafuta

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania ambapo aliwataka wananchi wa nchi za Uganda na Tanzania kuutumia mradi huu kwa manufaa ya nchi hizi mbili

Na. Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni wamewataka wananchi wa Tanzania na Uganda kuulinda, kuuenzi, kuuthimini na kuutumia mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghali kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania kwa faida na manufaa ya nchi zote mbili.

Wakizungumza katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba hilo huko katika kijiji cha Chingolieni, Mkoani Tanga leo, Marais hao walieleza kuwa mradi huo ambao ni wa pekee barani Afrika ni kielelezo cha udugu, urafiki na uhusiano mwema uliopo kati ya serikali na wananchi wa nchi hizo.

Rais Magufuli alimshukuru Rais Museveni kwa kuamua bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,445 lipite Tanzania kwani bado kulikuwa na nafasi ya bomba hilo kupitishwa mahala pengine ambako ni karibu zaidi na Uganda.

Alibainisha kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya majadiliano ambayo yaliyofanyika chini ya misingi ya ‘nipe ni kupe’ ambapo ilibidi Tanzania isamehe baadhi ya mambo ili kuwezesha mradi huo uweze kutekelezwa kwa faida na manufaa ya pande zote.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania ambapo alisema mradi huu uwe chachu ya kuimarisha uchumi ili kuwa na jumuiya imara ya Afrika Mashariki.

“Tulifanya ‘sacrifice’ ambayo itatupatia faida kubwa kwa Serikali na wananchi; tutapata ajira nyingi za kudumu na za muda, mapato usafirishaji wa mafuta, tutaweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo, yawezakana tukanunua mafuta ghafi hapa hapa badala ya kuagiza toa nje” alisema Rais Magufuli na kuwasisitizia wananchi kuwa Tanzania kama itakavyokuwa Uganda itafaidia sana na bomba hilo.

Katika hotuba yake hiyo Rais Magufuli alimhakikishia Rais Museveni kuwa bomba hilo litakuwa salama nchini Tanzania na kumueleza kuwa watanzania wako tayari kulilinda bomba hilo kwa kuwa wanaelewa ni kwa faida nchi zote mbili.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekubali rai ya Rais Museveni ya kutaka kujengwa kwa bomba mbadala kama hilo kwa ajili ya kusafirisha la gesi asilia inayochimbwa nchini kwenda Uganda ambayo inahitaji sana kwa ajili ya nishati ya kuzalisha chuma nchini humo.

“Yote yanawezekana, tumeanza vizuri, sisi tuliwakubalia na kwa hili hatuna sababu za kuwakatalia”alisisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli alieleza kuwa hivi sasa kuwa nchi hizo mbili ziko katika mazungumzo ili wataalamu wa mafuta kutoka nchini Uganda ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliofanikisha ugunduzi mafuta waweze kushirikiana na wataalamu wa Tanzania kufanya uchunguzi wa mafuta katika ziwa Eyasi na Tanganyika.

Rais Magufuli pia aliwatakadharisha wananchi ambao wako katika maeneo yanayopita bomba hilo kuacha kuendeleza maeneo hayo kwa dhamira ya kupatiwa fidia na kuwaonya kuwa watakaofanya hivyo hawatapatiwa fidia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali

“Tumeshapiga picha za maeneo yote yatakayopita bomba hilo. Wale wote watakaoguswa na ujenzi huo watalipwa fidia kwa mujibu wa sheria zilizopo” na kuonya kuwa wataoendeleza kwa dhamira kupata fidia “watakuwa wameula na chuya”akimaanisha hawataliwa.

Kwa upande wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseveni alimshukuru Rais Magufuli na Serikali ya Tanzania kwa kukubali kusamehe kodi na tozo mbali mbali ili mradi huo uweze kutekelezeka na kusisitiza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha udugu wa kweli kati ya nchi hizo.

“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kutuwezesha kutekeleza mradi huu. Tujihimu kufanya miradi mikubwa kama hii ili kujenga uchumi imara wan chi zetu na Jumuiya  imara ya Afrika Mashariki” Rais Museveni alieleza.

Katika hotuba yake hiyo Rais Museveni alisisitiza umuhimu wa kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi na kuahidi kuendelea  kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika miradi mingine zaidi.

Bomba la hilo la mafuta ambalo litagharibu dola bilioni 3.5 ambapo asilimia 80 ya ujenzi wake utafanyika Tanzania litapita katika mikoa nae nchini nane ambayo ni Kagera (katika wilaya za Misenyi, Bukoba vijijini, Muleba, Biharamulo), Geita (Geita, Chato, Bukombe na Mbogwe) Shinyanga (Kahama mijni, Tabora (Nzega, na Igunga), Singida ( Iramba, Mkalama na Singida Vijijini), Manyara (Kiteto  na Hanang), Dodoma( Kondoa na Chemba) na Mkoa wa Tanga (Kilindi, Handeni, Korogwe vijijini, Muheza na Tanga mjini.

8 thoughts on “JPM, Museveni Wawataka Wananchi Kutumia Fursa Bomba la Mafuta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama