Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Jitihada za Serikali na Sekta Binafsi Kutokomeza Kifua Kikuu

Na. Immaculate Makilika – MAELEZO

Ugonjwa wa kifua kikuu ni kati ya magonjwa matatu ikiwemo malaria na ukimwi yanayotokea sana kwa watu masikini duniani, ambapo asilimia 98 ya watu katika nchi zinazoendelea inaelezwa wameathirika na magonjwa haya.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ya mwaka 2007, inakadiriwa Tanzania ina jumla watu 120,191 wanaugua ugonjwa wa kifua, na ambapo wagonjwa ya zaidi 32,000 hufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.

Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 ambazo zimeathiriwa sana na ugonjwa huu, ambapo takwimu zinaonesha ya kuwa, ambapo takribani asilimia kati ya 30 na 50 ya watanzania wote tayari wameambukizwa Kifua kikuu.

Takriban watu 160,000 huugua kila mwaka na ni wagonjwa 62,180 sawa na 39% tu wanagunduliwa na kuwekwa katika matibabu ambapo kati yao asilimia 90 hupona kabisa.

Katika jitihada za kutokomeza Ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini, Serikali imeendelea kubuni mikakati mbalimbali ikiwemo kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo sekta binafsi kwa ajili ya kuongeza msukumo wa pamoja katika kudhibiti ugonjwa huo.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya mwaka 2018/19, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu anasema Wizara imeendelea na mkakati wake wa Udhibiti wa ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma ambapo katika kipindi cha Julai hadi Machi 2017, Serikali ilinunua na kusambaza dawa za Kifua Kikuu na Ukoma.

Anaongeza kuwa Kupitia ushirikiano wake na Wadau wa Maendeleo, Serikali imenunua  na kusambaza mashine za “genexpert” katika Wilaya zote nchini, hali ambayo imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za ugunduzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kutumia vipimo vya vinasaba.

“Nia  na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano  katika sekta ya Afya ni kushirikiana na sekta binafsi katika  mapambano dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu hasa kuongeza idadi ya wagonjwa wa TB wanaogunduliwa kutoka asilimia 40 hadi asilimia 70 mwaka 2020” anasema Waziri Ummy.

Waziri Ummy anasema Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo wamenunua na kusambaza mashine za “genexpert” 189  ikilinganishwa na mashine 66 zilizokuwepo mwaka 2015 pamoja jumla ya vitendanishi boksi 3,675 kwa ajili ya kusaidia katika ugunduzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kutumia vipimo vya vinasaba.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, mashine za  genexpert  zina uwezo wa kupima usugu wa dawa za kifua kikuu na wakati huo huo wa zitumika kupima makohozi, na hivyo kugundua kifua kikuu sugu kwa urahisi zaidi.

Waziri Ummy, anasema kuwa mashine hizi zimesambazwa kwenye hospitali zote za rufaa za kanda, mikoa, wilaya na baadhi ya vituo vikubwa vya afya nchini pamoja na hospitali binafsi tano (5) zilizopo jijini Dar es salaam ambazo ni Aga Khan, Hubert Kairuki, Regency Medical Center, TMJ na Hindul Mandal.

“Mashine hizo kila moja ina thamani ya shilingi milioni 38 za kitanzania, tumeanza na hospitali hizi zenye viwango vikubwa vya wagonjwa wanaohudumiwa na pia kwa kuzingatia utayari wa hospitali hizi katika kutoa huduma za kifua kikuu katika kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi wote” anasema Waziri Ummy.

Akifafanua zaidi anasema kuwa kipindi cha mwaka 2017 hadi Machi 2018 Serikali  imeongeza  vituo 41 na kufanya jumla ya vitu vinavyotoa huduma hiyo kufikia vituo 63 ikilingalishwa na kituo kimoja cha hospitali Maalum ya Kibong‟oto mwaka kilichokuwepo mwaka  2015.

Sekta binafsi ni wadau muhimu wanaopaswa kushirikiana kwa karibu zaidi na Serikali katika kutambua, kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa TB sambamba na kuongeza wigo wa huduma za matibabu ya wagonjwa wa kifua kikuu sugu nchini.

 

41 thoughts on “Jitihada za Serikali na Sekta Binafsi Kutokomeza Kifua Kikuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama