Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

JICA Yasaini Makubaliano Kusaidia Sekta ya Umeme.

Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) na Mkurugenzi kutoka JICA, anayeshughulikia masuala ya nishati, Hiroto Kamiishi (kulia) wakitia saini makubaliano ya msaada kutoka JICA kuwezesha sekta ya nishati nchini.

Na Veronica Simba – Dodoma

Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati, wametia saini makubaliano ya msaada kutoka Shirika hilo utakaowezesha Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hususan katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji na usafirishaji wa umeme.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo mjini Dodoma, kati ya Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, akiwakilisha Serikali na Mkurugenzi kutoka JICA, anayeshughulikia masuala ya nishati, Hiroto Kamiishi.

Akielezea kuhusu mafunzo husika, Kamishna Luoga amesema kuwa, yanalenga kuwaongezea uwezo wahandisi na mafundi mchundo na kwamba yatatolewa kwa njia ya vitendo, hivyo mbali ya kutoa elimu pia miundombinu husika katika nchi nzima itakarabatiwa.

 

Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) na Mkurugenzi kutoka JICA, anayeshughulikia masuala ya nishati, Hiroto Kamiishi (kulia) wakipeana mikono baada ya kutia saini makubaliano ya msaada kutoka JICA kuwezesha sekta ya nishati nchini.

Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), wakiwa katika kikao na Wataalam wa Nishati kutoka Tanzania (hawapo pichani), kabla ya pande hizo mbili kutia saini makubaliano ya msaada kutoka JICA kuwezesha sekta ya nishati nchini.

Sehemu ya wataalam wa Nishati kutoka Tanzania wakiwa katika kikao na Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), (hawapo pichani), kabla ya pande hizo mbili kutia saini makubaliano ya msaada kutoka JICA kuwezesha sekta ya nishati nchini.

“Mradi huu umelenga zaidi kusaidia kuondoa tatizo la upotevu wa umeme wa kiufundi (technical losses) na hivyo kusaidia TANESCO kuongeza mapato,” amefafanua.

Akifafanua zaidi, Kamishna Luoga ameeleza kuwa, hii ni awamu ya pili ya Mradi husika ambayo ni ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2018 hadi 2021. “Katika mwaka wa kwanza, Mradi utatekelezwa katika Mkoa wa Dar es Salaam na miaka miwili utatekelezwa katika Mikoa mingine yote nchini.”

Aidha, Kamishna Luoga (kwa niaba ya Serikali) amewashukuru JICA kwa misaada na mikopo wanayotoa katika kuwezesha miradi mbalimbali ya sekta ya nishati nchini ikiwa ni pamoja na Mradi mkubwa wa Backbone, Mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Singida Tanzania hadi Isinya Kenya, pamoja na Mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa megawati 300 ulioko Mtwara.

“Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO, inaahidi kutoa ushirikiano katika kutekeleza Mradi huu na mingine yote, amesisitiza.”

Awamu ya kwanza ya Mradi huu, ambayo pia ilifadhiliwa na JICA ilitekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

8 thoughts on “JICA Yasaini Makubaliano Kusaidia Sekta ya Umeme.

 • August 10, 2020 at 2:05 am
  Permalink

  This page really has all of the information and facts I needed about this subject and didn’t know who to ask.

  Reply
 • August 12, 2020 at 6:41 am
  Permalink

  Yesterday, while I was at work, my sister stole
  my apple ipad and tested to see if it can survive a 30
  foot drop, just so she can be a youtube sensation. My apple ipad is now destroyed and she has 83 views.

  I know this is completely off topic but I had to
  share it with someone! adreamoftrains web hosting sites

  Reply
 • August 24, 2020 at 11:30 pm
  Permalink

  I am really inspired together with your writing abilities and
  also with the layout on your weblog. Is this a paid subject or did you customize it your self?
  Anyway stay up the nice high quality writing, it’s rare to look
  a nice blog like this one today.. cheap flights
  34pIoq5

  Reply
 • August 26, 2020 at 7:18 am
  Permalink

  It’s very easy to find out any topic on web as compared to textbooks, as I found this piece of writing at this site.

  Reply
 • August 27, 2020 at 12:42 pm
  Permalink

  I am extremely impressed along with your writing abilities and
  also with the format on your weblog. Is that this a paid
  theme or did you modify it yourself? Either way stay up the excellent
  quality writing, it is uncommon to see a great weblog like this one today..

  Reply
 • August 28, 2020 at 6:13 pm
  Permalink

  You have made some really good points there.
  I looked on the web for more info about the issue
  and found most people will go along with your views on this web
  site.

  Reply
 • September 5, 2020 at 10:44 am
  Permalink

  Quality posts is the crucial to invite the visitors to pay a quick visit the web site, that’s what this website is providing.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama