Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Jeshi la Polisi Latakiwa Kujenga Uchumi wa Kisasa

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Viongozi wa Majeshi na Serikali pamoja na Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018

Na.Immaculate Makilika – MAELEZO

Jeshi la Polisi nchini limetakiwa  kuwa na mwelekeo mpya  wa kujenga uchumi wa kisasa, kwa kushiriki katika shughuli za ujenzi wa viwanda sambamba na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya ujenzi wa viwanda na kufikia nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

Akizungumza  leo jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuwatunuku vyeo wahitimu 513  waliofaulu zaidi mafunzo ya  Uofisa na Ukaguzi, katika Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es salaam, Rais Magufuli alisema kuwa imefika wakati Jeshi  la Polisi kuwa na mwelekeo mpya wa uchumi wa kisasa ili kusaidia majeshi hayo kuwa na uwezo wa kujiendesha vizuri bila kutegemea sana Serikali.

“Mtafute mwelekeo mpya wa majeshi yetu, unaolenga kujenga uchumi wa kisasa, mjipange kushiriki shughuli za uchumi hasa ujenzi wa viwanda, pamoja na kupanua wigo wa kutengeneza sare zenu, na bidhaa mbalimbali za viatu au maji hali itakaosadia kuwa na bidhaa za ziada badala ya kununua  na kuweza kujiendesha” alisema Rais Magufuli

Rais Magufuli alitolea mfano baadhi ya majeshi kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo barabara ,ambapo alisema  Jeshi la nchi ya China  limejenga mji mkubwa nchini humo.

Aidha, Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Magereza kushirikiana na majeshi mengine nchini likiwemo Jeshi la Polisi kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali pamoja na kusaidiana masuala kadhaa.

Sambamba na hilo, Rais Magufuli ameahidi kukipatia Chuo cha Taaluma ya Polisi nchini kiasi cha shilingi milioni 700 kabla ya ijumaa wiki ijayo kwa ajili ya kukarabati chuo hicho kwa kujenga mabweni na madarasa ya kisasa kwa lengo la kuboresha hali ya chuo na kuongeza ufanisi kwa wahitimu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, alisema  ujenzi wa makazi ya Polisi unaendelea kwa kutumia fedha walizopewa  na Serikali kiasi cha shilingi bilioni 3.7, na wanatarajia  kukarabati nyumba 400 za Polisi mara baada ya kupewa kiasi cha fedha kilichobaki ikiwa ni  ahadi ya Rais Magufuli, aliyoitoa mapema mwaka huu ya kuwapa  Jeshi hilo shilingi bilioni 10 ambazo ameahidi kuwapa ndani ya  kipindi cha wiki moja.

Vilevile, IGP Sirro, alisema kuwa nchi iko salama kwani hali ya uhalifu imepungua kwa kuwa Jeshi la Polisi  limeendelea kufanyakazi kwa kuzingatia nidhamu na weledi

“Hali ya uhalifu imepungua nchi nzima,makosa ya barabarani yamepungua kwa asilimia 32.6, ajali zimepungua kwa asilimia 30.8, kwa ujumla kumekuwepo na upungufu wa matukio ya uhalifu kwa sababu Jeshi la Polisi linashirikiana na wananchi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao”alisema IGP Sirro

Naye, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi, Anthony Rutashugurugukwa, alisema kuwa  mafunzo hayo yanayotolewa kwa lengo la kupanda daraja na vyeo  yalidumu kwa muda wa miezi sita, ambapo wanafunzi 513 walihitimu masomo hayo yaliyogawanyika katika  sehemu mbili za mafunzo ya Ukaguzi na Uofisa. Wahitimu wa mafunzo ya Uofisa walikuwa 120 ikiwa wanaume 106 na wanawake 14. Aidha, katika mafunzo ya Ukaguzi kulikuwa na wahitimu wanaume 393 na wahitimu wanawake 60.

Naibu Kamishna huyo wa Polisi alisema kuwa wahitimu hao wamepata mafunzo mbalimbali yakiwemo stadi za upelelezi, medani za kivita na masuala mengine mtambuka.

 

4 thoughts on “Jeshi la Polisi Latakiwa Kujenga Uchumi wa Kisasa

 • August 11, 2020 at 11:18 pm
  Permalink

  Asking questions are in fact pleasant thing if you are not understanding something totally, however this article gives nice understanding yet.

  Reply
 • August 14, 2020 at 4:29 am
  Permalink

  First of all I want to say superb blog! I had a quick question in which I’d like to ask if you don’t mind.

  I was interested to find out how you center yourself and clear your thoughts
  before writing. I have had a hard time clearing my thoughts in getting my ideas out there.
  I truly do take pleasure in writing however it just seems like the first 10 to 15 minutes are lost
  just trying to figure out how to begin. Any suggestions or hints?
  Many thanks!

  Reply
 • August 26, 2020 at 12:31 am
  Permalink

  Thanks for the auspicious writeup. It if truth be told was
  once a leisure account it. Look complex to far added
  agreeable from you! By the way, how can we keep in touch?
  yynxznuh cheap flights

  Reply
 • August 27, 2020 at 1:52 pm
  Permalink

  Greetings! Very helpful advice within this article! It’s the little changes that produce the biggest changes.
  Many thanks for sharing!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama