Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

JAMAFEST – Ulaji Mwingine Huo kwa Wafanyabiashara Tanzania

Na Judith Mhina-Maelezo

Tanzania ina jukumu la kuandaa Tamasha la Jumuia ya Afrika Mashariki- JAMAFEST, likiwa ni tamasha la Nne ambalo limetanguliwa na yale yaliyofanyika katika nchi za nchi za Kenya, Rwanda na Uganda.

Tamasha la JAMAFEST litaanza tarehe 21 mpaka 28 Septemba 2019 na linakadiriwa kuhudhuriwa na zaidi ya wageni laki (100,000) moja na zaidi ambao, mpaka sasa wamejiandikisha na kufanyika katika Uwanja wa Taifa uliopo Wilaya ya Temeke Dar-es-salaam.

Hakika, hiki ni kipindi cha kufanya bishara kwa wafanyabiashara, wajasiriamali, mama na baba lishe, wenye usafiri kama taxi, bajaji, wenye nyumba za wageni na hoteli   ndogo za kati na kubwa. Neema hii ya ujio wa wageni ni fursa kubwa kwetu tuitumie kwa kuwa wakarimu, ii kuwavutia na kupendekezwa kwa masuala mengi yakimataifa yafanyike Tanzania.

Aidha, washiriki wa Tamasha hilo watakaoshiriki hapa nchini kama vile, wenye saloon, wasusi, wana mitindo wasanii wa filamu, wachonga vinyago wachoraji,  wana muziki , watunza bustani za wanyama, wakuna nazi,  vyakula vya jadi, ufinyanzi, watapewa mabanda ya kufanya na kuonyesha kazi zao bila malipo yoyeto ili mradi umejisajili.

Pia, Michezo kama michezo mbalimbali ya watoto na shughuli za watoto ikijumuisha kucheza, kuchora kwa rangi, kuchora kwa kalamu, utengenezaji wa sanamu, kuimba, kupiga na kucheza ngoma, kupiga ala, kuigiza, ushairi, mdahalo (debate) na mashindano ya uandishi wa insha kwa kufuata Kaulimbiu ya Tamasha. “Uanuai wa Kitamaduni: Msingi wa Utangamano wa Kikanda, Maendeleo ya Kiuchumi na Kushamiri kwa Utalii” (Cultural Diversity: A Key Driver to Regional Integration, Economic Growth and Promotion of Tourism). Michezo mengine ni kama vile kukuna nazi, rede, kuvuta kamba, tikri, mieleka, kucheza bao, kukimbiza kuku na kukimbia kwa magunia

Wengine watakaofaidika ni maonyesho ya picha jongefu na makala, maonesho ya picha mnato, dawa za jadi, ulibwende, vinywaji vya jadi,  machapisho na kazi za fasihi andishi, wenye kuhitaji banda la wanyama na bidhaa zote za wajasiriamali na wabunifu.

Shangwe na vifijo hivyo vya kufanya biashara unatokana na nchi tano za Jumuia ya Afrika Mashariki kudhibitissha ushiriki wake ambazo ni Tanzania wenyeji, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Jmhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Dira ya Tamasha la JAMAFEST ni kuiunganisha Afrika Mashariki kupitia Sanaa na Utamaduni, ambapo dhima kuu ni kuwa na utangamano wa kikanda ulioshamiri kupitia Sanaa na Utamaduni. Lengo likiwa ni kuchochea kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia ukuzaji wa sekta za ubunifu na Utamaduni.

Vilevile, JAMAFEST linatoa jukwaa la kuonyesha Utamaduni kama msukumo madhubuti wa utangamano na maendeleo ya kikanda. Kuwaleta na kuwaunganisha pamoja wadau na viongozi wa sekta, kuendeleza na kuenzi urithi wa utamaduni wetu.

Hii inaimarisha kutoa fursa ya majadiliano ya kitaaluma baina ya wananchi wa Afrika Mashariki, kutumia utamaduni na ubunifu kama nyenzo ya kuenzi na kukuza utambulisho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutangaza fursa na rasilimali za kipekee ilizonazo nchi yetu.

Akifahamisha  ujio wa JAMAFEST  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema ni matambezi ya kitamaduni, (Carnival) ambapo kila nchi mwanachama itakuwa na eneo lake la kuonyesha ubunifu sanaa na tamaduni za nchi katika siku ya ufunguzi.

“Tukio hili ni la kuvutia sana na lina toa nafasi kwa wananchi wa jiji la Dar es salaam na Viunga vyake kujionea fursa hizi za kiutamaduni na Sanaa. Pia ni fursa ya kibiashara natambua wenye taxi, maji na hoteli watafanya biashara kubwa katika matembezi haya na pia wakati wa shuhuli za tamasha. Kwa wana habari mtapata maudhui ya kipekee katika kipindi hiki. Amesema Mwakyembe

Waziri Mwakyembe ameongeza kwa kusema kuwa kutakuwa na maonesho ya Jukwaani (Performances) ambayo yatahusisha; Muziki, Ngoma Ushairi, Hadithi, Tamthilia, Michezo ya Kuigiza, Sarakasi na Vichekesho.

Aidha, siku zote nane zitapambwa na fani mbalimbali katika maeneo mbalimbali. Nchi wanachama zitaleta vikundi, uchezi, bendi za muziki michezo ya kuigiza ushairi n a mengine yanayofanana na hayo.

Wito kwa wenye bidhaa bora wabunifu waione fursa kwa njia adhimu ya kushiriki na pia kwa watanzania ni nafasi ya kupata bidhaa zitokazo katika hizi sita. Tunawasiliana na wenzetu wa wizara ya maliasili na utalii kuona namna bora ya kutumia maonyesho ya wanyama hai (Zoo), Amesisitiza Waziri Mwakyembe.

Akifafanua kuhusu maonesho ya vyakula vya jadi kwa Nchi Wanachama. Waziri Mwakyembe amesema kuwa pia, wajasiriamali watauza vyakula vya jadi Traditional Food Market and Exhibition.

Hivyo, milango iko wazi kwa wanaopenda kufanya maonyesho na biasghara ya vyakula vya asili. Tayari kati washiriki wapo ambao wameomba kuprwa fursa hizo., kwa wataohitaji kutoa huduma hiyo manahimizwa kujisajili na kuwasilisha maombi kwa ajili ya utoaji wa huduma hiyo. Katika siku ya matembezi ya kiutamaduni jioni yake kupitia tammasha la Urithi tunashirikiana nao kutakuwa nyama choma asilia. )nisimalize uhondo la muhimu watanzania wasikose kuja kutembea maonyesho na wanapenda kushiriki basi wasikose fursa hii adhaimu. Tamasha litakuja tena Tanzania 2031

Akielezea kuhusu Ziara, Tuzo na Utalii Cultural Excursion, Awards and Tourism.katika kukuza na kutangaza utalii wa asili na wa kiutamaduni kutakuwa na ziara kwa mshiriki mmoja kutoka kila Nchi Mwanachama kutembelea  hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Saadan maporomoko ya Udzungwa. Aidha washiriki wote watakaopenda kutembelea Makumbusho ya Taifa, Kijiji cha Makumbusho, Magofu ya Kale ya Bagamoyo, hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Saadani, Soko la Vinyago la Mwenge na Kariakoo wametengewa siku za kufanya ziara.

Vilevile kwa upande wa upandaji wa Mlima Kilimanjaro kila Nchi Mwanachama itatoa mshiriki mmoja na washiriki watakaofanikiwa kufika kwenye kilele watapewa tuzo wakati wa usiku wa kilele cha tuzo Kwa kishirikiana na Tamasha la Urithi   tuzo za Insha wanafunzi; Miss JAMAFEST; fashion; kundi maalum katika ubunifu; walio na mchango katika  utalii wa kiutamaduni; waandishi wa habari za utamaduni na Sanaa; upandaji Mlima Kilimanjaro; Makala za filamu za Utamaduni.

Pia, Utalii, na Historia: Sanaa za Ufundi na Muziki zitaendeshwa  kwa kushirikisha nchi Insha Filamu na Sanaa kama nilivyoeleza.  Tuzo za washindi wa insha kwa wanafunzi watatu (3) kutoka kila nchi zinalenga insha zilizotumia Kaulimbiu ya Tamasha na kushinda.Tuzo zote zinalenga kutangaza nchi yetu katika nyanja za Utamaduni, Ubunifu Sanaa na Utalii

Akimalizia  Waziri Mwakyembe ameyataja maonesho ya mavazi na ulimbwende Fashion Show and Modeling.kuwa kutakuwa na maonesho ya mavazi na ulimbwende kutoka kwa kila Nchi Mwanachama na mshindi atatwaa Taji la Miss JAMAFEST TANZANIA, 2019. Pia maonyesho ya fasheni ambapo tutashitikisha pia makundi maalum.

Watanzania wafanyabiashara na wajasiriamali wa aina yeyote ile chukua hatua jongea na kushirikiana a watanzania wengine katika kujiineemesha wewe mwenyewe binafsi pamoja na familia yako. Lakini utambue unaposhiriki na Taifa linanufaika kwa njia moja au nyingine.

Hakikisha unajisajili kwa kutumia njia ya mtandao na iwapo unaona huwezi kutumia mtandao kwa wale wa Dar-es-salaam na Viunga vyake wanaweza kufika uwanja wa Taifa – Temeke na kuuliza Idara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ofisi zao, ili kukutana na wawakilishi wa Idara ya Utamaduni waweze kupewa fomu na kujisajili.

Mwitikio na tabia iliyojitokeza katika kipindi cha ujio wa wageni wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika yaani –SADC WAKATI WA Mkutano wa 39 wa viongozi wa jumuia hiyo, ni vema ikaonekana katika ujio wa JAMAFEST – Mungu ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika Mashariki.

307 thoughts on “JAMAFEST – Ulaji Mwingine Huo kwa Wafanyabiashara Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama