RAIS Dkt. John Magufuli amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu pamoja na kutambua nafasi, wajibu na majukumu yake ili kuepuka mgongano na mihimili ya Dola.
Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha Viongozi na Watendaji mbalimbali wa Serikali aliowateua mwishoni mwa wiki, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Jumatatu (Novemba 4, 2019), Rais Magufuli alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anapaswa kutambua wajibu wake na kutek...
Read More