Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip I. Mpango
UTANGULIZI
Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kuendelea kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha wote kukutana tena hapa Jijini Dodoma, kupokea Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2020/21. Wasilisho hili ni kwa mujibu wa Kanuni ya 97 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016. Aidha, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuijalia...
Read More