Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Ripoti ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kijiji cha Chikundi wakati wa Mkutano wa wadau kujadili utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Ruangwa Pride wilayani Ruangwa, Lindi tarehe 22 Machi, 2024. Mkutano huo umebebwa na kaulimbiu isemayo; “Usawa wa Kijinsia katika Umiliki wa Ardhi kwa Ustawi wa Jamii”. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geofrey Pinda na katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma.
Read More