Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (hawapo pichani) ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya viwanda na biashara, uwekezaji, na masuala ya kodi. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na wataalamu waandamizi kutoka Wizara hizo.
Read More