Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Zingatieni Mabadiliko ya Maisha Baada ya Kustaafu- Mwaluko
Jun 17, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_44488" align="aligncenter" width="822"] Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Doroth Mwaluko akifungua mafunzo kwa watumishi wa Ofisi hiyo wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Watumishi wanaotarajia kustaafu wameaswa kuzingatia mabadiliko ya maisha kutoka katika utumishi wa umma kwenda katika mfumo wa maisha ya  kawaida na kujiepusha kufanya miradi ambayo hawana ujuzi wa kutosha kuihusu.

 Akizungumza katika mafunzo kwa yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni ili wawe na mbinu za kuendana na mazingira hayo, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko amesem kuwa Ofisi hiyo inatambua umuhimu wa wastaafu na faida za kujiandaa kustaafu.

“ Kuna umuhimu mkubwa wa kutambua kuwa suala la kustaafu ni la kila mmoa wetu na ni muhimu kujiandaa vyema na maisha mapya ambayo kimsingi yatakuwa tofauti na haya ya utumishi wa umma mliyo nayo  kwa sasa” Alisisitiza Mwaluko

[caption id="attachment_44489" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Doroth Mwaluko akisisitiza umuhimu wa mafunzo  kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa kila mtumishi wa umma lazima atambue kuwa ni mstaafu matarajiwa hivyo kujiandaa kwake ni jambo  muhimu.

Kwa upande wake Muwezeshaji Kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Jijini Dar es Salaam Bw. Peter Seme amesema kuwa watumishi hao wanaotarajia kustaafu watajifunza mambo mengi yakuwawzesha kuendelea na maisha yao kama kawaidia hata baada ya kustaafu.

Alitaja baadhi ya mada kuwa ni pamoja na utayari wa kupokea mabadiliko baada ya kustaafu, Stadi za kuongeza kipato, Mtindo wa maisha bora baada ya kustaafu, Namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu.

[caption id="attachment_44490" align="aligncenter" width="841"] Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bi Mazoea Mwera akizungumza wakati wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi hiyo wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake mmoja wa watumishi hao  Bw. Esamo Sawaki amesema kuwa  wanaipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi hiyo ili waweze kukabiliana na changamaoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kupata uzoefu kutoka kwa wastaafu wengine ambao tayari wana uzoefu katika kukabiliana na changamoto za kustaafu na hata kuelewa kazi ambazo ni za uzalishaji wanazoweza kuzifanya kama wastaafu ili kuwaletea tija.

“Tutapata maarifa sahihi ya namna ya kutumia kiinua mgongo tutakachopewa baada ya kustaafu kutoka katika utumishi wa umma” Alisisitiza  Sawaki

Mafunzo yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni yanafanyika Jijini Dodoma kwa siku tano yakiwashirikisha watumishi hao kutoka kada mbalimbali.

[caption id="attachment_44491" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za Bima Tanzania Kanda ya Kati Bi Monica Robert akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_44492" align="aligncenter" width="882"] Muwezeshaji kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Bw. Peter Seme akizungumza katika mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_44487" align="aligncenter" width="868"] Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Doroth Mwaluko (Katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma mara baada ya kufungua mafunzo hayo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kustaafu.[/caption]

(Picha na Frank Mvungi- Dodoma)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi