Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Zimbabwe Kuendelea kuimarisha uhusiano  na Tanzania
Jun 28, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33132" align="aligncenter" width="600"] Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.[/caption] [caption id="attachment_33129" align="aligncenter" width="600"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Zimbabwe zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya Rais huyo wa Zimbabwe kuwasili nchini.[/caption]

Na. Immaculate Makilika –MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangangwa  amesema serikali yake itaendelea kushirikiana  na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania  ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo, Rais Mnangagwa  amesema kuwa Tanzania imesaidia kwa kiasi kikubwa katika harakati za ukombozi wa nchi za Zimbabwe, Afrika  Kusini, Namibia na Msumbiji na hivyo ni jukumu lao kuimarisha uhusiano huo mzuri.

“Sisi kizazi cha zamani ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunakieleza kizazi cha sasa kuhusu  jitihada za Tanzania katika harakati za ukombozi  wa nchi za kusini mwa Afrika”

“Tulikuwa tunakuja hapa, jengo hili na Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wakati huo, ambapo aliweza kusuluhisha migogoro iliyokuwepo kati ya chama cha ZANU na ZAPU” aliongeza Rais Mnangangwa.

Rais Mnangagwa alisema kuwa serikali yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali yatakayosaidia kukuza uchumi wake na kuahidi kuwa  baada ya Uchaguzi Mkuu kuisha utaotarajiwa kufanyika Julai 30 mwaka huu, Tume ya Ushirikiano itakutana kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo ya kibiashara.

[caption id="attachment_33130" align="aligncenter" width="626"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alisema Tanzania  na Zimbabwe ni nchi marafiki tangu harakati za uhuru mwaka 1960.

Ambapo  mwaka 1982  ilianzishwa Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe  kupitia taasisi mbalimbli za kimataifa ikiwemo SADC.

Aidha, Rais Magufuli ametaja mikakati ya  kukuza na kuimarisha ushirikiano wa uchumi  katika maeneo ya sita ambayo ni   biashara ambapo nchi hizo zimedhamiria kutumia fursa za SADC za kulegeza masharti ya biashara.

[caption id="attachment_33131" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam[/caption]

Maeneo mengine ni  la kukuza uwekezaji , utalii, usafiri wa anga na barabara, kushirikiana kupitia SADC kwa maana ya fursa za wanachama. Pamoja na eneo la ulinzi, usalama, afya, utamaduni, sanaa na michezo.

Vilevile, Rais Magufuli amesema wanawakaribisha Wazimbabwe kuja kuwekeza nchini Tanzania hasa ukizingatia kwamba kuna kiwango kidogo cha uwekezaji baina ya nchi mbili ambazo ni marafiki wa muda mrefu.

[caption id="attachment_33133" align="aligncenter" width="900"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha pamoja na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

“Mwaka 2006 kiwango cha uwekezaji cha Zimbabwe nchini kilikuwa na thamani ya biashara ya sh. bilioni 18.3, huku mwaka 2017 ikiwa sh. bilioni 21.1, hivyo tumekubaliana kuimarisha baadhi ya maeneo ili kuleta mkakati wa kuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili” alisema Rais Magufuli.

Rais Mnangagwa ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, kesho juni 29 anatarajiwa kutembelea Chuo cha Sanaa cha Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika. Ambapo  Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi