Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Zabuni Mradi wa Umeme Rufiji zafunguliw
Feb 02, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28429" align="aligncenter" width="750"] Wataalam kutoka Idara ya Manunuzi, Wizara ya Nishati wakifungua nyaraka mbalimbali za zabuni katika kikao hicho kilichofanyika Wizarani leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Zabuni kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji zimefunguliwa  leo tarehe 02 Februari, 2018.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zabuni hizo kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon MacAchayo amesema zabuni hizo ni za Awamu ya Pili kutokana na kukosekana kwa mshindi katika Awamu ya Kwanza iliyotangazwa mapema mwaka jana.

Alisema kuwa, katika awamu ya kwanza jumla ya kampuni 81 zilinunua nyaraka za zabuni ambapo nakala moja ilikuwa inauzwa kwa shilingi 200,000 lakini ni kampuni nne tu zilifanikiwa kurejesha maombi na kuongeza kuwa kampuni zote nne hazikuwa na  vigezo vinavyohitajika hali iliyopelekea kutangazwa upya kwa zabuni tarehe 19 Desemba, 2017 katika vyombo vya habari  vya ndani na nje ya nchi.

[caption id="attachment_28430" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon MacAchayo (mbele) akizungumza na wawakilishi wa kampuni mbalimbali zilizoomba zabuni kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji kwenye ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam leo[/caption]

MacAchayo aliongeza kuwa, katika awamu ya pili kampuni 17 zilijitokeza katika ununuzi wa nyaraka kwa gharama ya shilingi 500,000 kwa kila moja ambapo mpaka siku zinafunguliwa ni kampuni tano tu zimerejesha nyaraka zenye maombi ya zabuni.

Alisema hatua inayofanyika kwa sasa ni ufanyaji wa tathmini ya zabuni hizo na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa tathmini ya zabuni hizo waombaji wote watajulishwa mshindi na baada ya hapo zitafuata taratibu za mazungumzo, barua na kuandaa mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi mara moja.

Aliwataka kampuni zilizowasilisha maombi kuwa watulivu wakati zoezi la tathmini likiendelea.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi