Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wizara Yakutana na Wadau Kupitia Sera ya Wanawake na Jinsia
Aug 09, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_8763" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akizungumza na wadau wa Maendeleo ya jinsia wakati walipokutana kujadili maboresho ya Sera ya Maendeleo ya jinsia na Wanawake mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi na kulia ni Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Maseli Katemba.[/caption]

Na: Eliphace Marwa –MAELEZO

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na  wadau wa masula ya jinsia jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupitia Sera ya Mendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 ili kuiboresha kwa kuzingatia mahitaji ya sasa.

Akifungua kikao hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga alisema kuwa ushiriki wa wadau kutoka ngazi ya Halmashauri ni wa muhimu ili kuibua maoni ya wananchi yatakayosaidia kuboresha sera iliyopo sasa.

 “Ushiriki wa wadau ni muhimu kwani ninyi ndio mnaosimamia utekelezaji wa Sera na mikakati ya Sera katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri maoni na changamoto mnanazotukutana nazo ni muhimu ili kujumuisha katika kipindi hiki cha kuhuisha Sera hii” alisema Bibi Sihaba.

[caption id="attachment_8764" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akifafanua jambo kwa wadau wa Maendeleo ya Jamii wakati walipokutana kujadili Sera ya Maendeleo ya Jinsia na Wanawake mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga.[/caption]

Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Maendeleo ya Jamii toka Mkoani Iringa Bi. Saida Mgeni amesema kuwa Sera pendekezi itawezesha kufanya tathimini itakayotoa mwelekeo kwa kuona kuwa mipango na mikakati mbalimbali inazingatia mambo muhimu yanayohimiza jamii kuachana na mitazamo ya kuwatambua wanawake peke yao, na badala yake kutambua ushiriki wa wanaume kama wadau muhimu katika Sera hii.

Bi. Mgeni, aliongeza kuwa Sera inayopendekezwa itahimiza ushiriki sawa wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi, upatikanaji wa haki sawa kwa wanawake, uwepo wa hifadhi za jamii, kupunguza mzigo wa kazi, kuwashirikisha wanawake katika shughuli za kiuchumi pamoja na kuwahusisha wanawake katika fursa mbalimbali ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

[caption id="attachment_8765" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wadau wa maendeleo ya Jinsia wakiendelea na mkutano wakati walipokutana kujadili maboresho ya Sera ya Maendeleo ya jinsia na Wanawake mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa)[/caption]

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi alibainisha kuwa sera hii itawanufaisha wavulana na wasichana, wanawake na wanaume kwani hivi sasa watoto wengi wa kike katika elimu ya juu wamekuwa hafanyi vizuri hasa katika masomo ya sayansi.

Aidha wadau wameipongeza Wizara kwa uamauzi wake wa kuwashirikisha wadau wa ngazi zote ili kupanua wigo wa maoni kutoka ngazi mbali mbali kwa ajili ya umiliki wa sera hiyo na uzingatiaji wa haki za kijinsia ili kufanikisha azma ya Serikali ya kuwa na maendeleo endelevu kwa wanawake hapa nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi