Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wizara ya Ardhi Yafanya Maboresho Katika Kitengo Cha Usajili wa Hati
Sep 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_11584" align="aligncenter" width="750"] Msajili wa Kitengo cha Hati; Bw. Kastor Ngonyani akizungumzia Maboresho yaliyofanyika katika ofisi yake.[/caption]

Kitengo cha Usajili wa Hati na Nyaraka katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kimefanya maboresho katika upatikanaji wa Hati na Nyaraka kwa muda mfupi zaidi na ilivyokuwa hapo awali.

Akizungumza wizarani hivi karibuni; Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hati; Bwn. Kastor Ngonyani alisema; Katika zoezi la usajili wa Hati mpya zilizokuwa zikiandaliwa kwa muda wa miezi mitatu toka tarehe ya kuwasilishwa kwa Msajili, sasa zoezi hilo linachukua wiki mbili tu. Ameeleza utaratibu huo umerahisishwa kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki.

Aidha, Bwn. Ngonyani alisema kwa nyaraka nyingine zinazohusu Ardhi, kama zile za Uhamisho, Mikopo na zile zisizohusu Ardhi/za mali zinazohamishika zinatumia wiki moja tu kuwa tayari kutoka tarehe ambapo nyaraka husika iliwasilishwa kwa Msajili wa Hati.

[caption id="attachment_11585" align="aligncenter" width="750"] Afisa katika Kitengo cha Hati akimhudumia mteja aliyefika katika dawati lake.[/caption]

Vile vile, Msajili alisema kwamba utoaji wa taarifa nyingine za upekuzi/ Search ambazo huhusisha taarifa mbalimbali kama vile; Kujua kiwanja ni cha matumizi gani, kina Hati au hakina, Mmiliki wake ni nani na taarifa zinazofanana na hizo kuhusu Historia ya kiwanja husika; " Sasa taarifa hizo zinapatikana kwa siku mbili tu, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo zoezi hilo lilikuwa linachukua wiki mbili, mwezi mzima au hata zaidi," alisema Bwn. Ngonyani.

[caption id="attachment_11588" align="aligncenter" width="750"] Maafisa mbalimbali katika Kitengo cha Hati. Na wengine wa Idara mbalimbali za Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiendelea kuhudumia Wananchi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja Wizarani hapo.[/caption]

Bwn. Ngonyani alieleza jinsi ambavyo ofisi yake imekuwa na Hati na nyaraka mbalimbali za Wananchi ambao bado hawajafika kuchukua Hati na Nyaraka hizo, licha ya nyaraka hizo kuwa tayari kwa muda mrefu uliopita. Bwn. Ngonyani alitoa rai kwa Wananchi wote ambao walishafika katika ofisi yake kwa ajili ya kupatiwa huduma hizo wafike kuchukua Hati na Nyaraka hizo muhimu kwao.

Ofisi ya Kitengo cha Msajili wa Hati ipo kisheria . Sheria zinazoainisha  uwepo wake sambamba na majukumu yake ni ; Sheria ya Usajili wa Ardhi , Sura ya  334 ya Sheria za Nchi; Sheria ya Usajili wa Nyaraka, Sura 117 ya Sheria za Nchi;  Sheria ya Uhamisho wa Mali/Usajili wa Mali zinazohamishika, Sura 210 ya Sheria za Nchi na Sheria za Usajili wa Majengo ( Unit Tittle  Act).

Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi