[caption id="attachment_1984" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti kutoka Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Radhimina Mbilinyi akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam leo (jana).[/caption]
Na Benjamin Sawe.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao.
Akizungumza katika semina hiyo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, Radhimana Mbilinyi amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi.
“Ni muda muafaka kwa waajiri kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia kutambua madhara ya kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Bi. Mbilinyi.
[caption id="attachment_1987" align="aligncenter" width="750"] Afisa Matekelezo Mwandamizi kutoka Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa mada katika semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam leo (jana).[/caption]Katika hotuba yake, Bi Mbilinyi alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatapo majanga wakiwa kazini.
Akizungumza wakati akitoa mada, Afisa Matekelezo Bi. Amina Likungwala amesema Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa waajiri kwa kutambua kuwa waajiri ndio wadau wakuu wa Mfuko huo na semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.
[caption id="attachment_1990" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Abdullssadaam Omary akitoa mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam leo (jana).[/caption] [caption id="attachment_1993" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa semina ya uelimishaji kwa waajiri wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa semina hiyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bi. Radhimina Mbilinyi jijini Dar es Salaam leo (jana).[/caption]Nae, Afisa Madai wa Mfuko huo, Bi Grace Tarimo, alisema Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.