Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Zungu: Mapato ya mfuko wa mazingira yaainishwe kwenye sheria
Jun 12, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53193" align="aligncenter" width="750"] Serikali ya Awamu ya Tano inatajwa kuchochea mageuzi katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini na hivyo kuongeza ustawi wa wananchi katika maeneo ya Vijijini na Mijini.[/caption]

Na Mwandishi Wetu- VPO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema ipo haja ya kuanisha vyanzo vya mapato ya mfuko wa mazingira kwenye sheria ili kuongeza wigo katika usimamizi wa mazingira.

Zungu amesema hayo leo alipokutana na wadau wa mazingira kutoka Jukwaa la Kilimo pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ofisini kwake jijini Dodoma.

Alisema kwa kuanisha kazi hizo kwenye sheria kutasaidia kuwafanya wananchi wawe sehemu ya kuboresha na kuhifadhi mazingira badala ya kuachia Serikali peke yake.

[caption id="attachment_53194" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na wadau wa mazingira kutoka Jukwaa la Kilimo Tanzania pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ofisini kwake jijini Dodoma leo.[/caption]

Waziri Zungu aliongeza kuwa alipendekeza kuwepo kwa na chanzo cha mapato yanayotokana na uchafuzi kupitia vyombo vya moto kwa kuwa hivi sasa upo utaratibu wa kutoza ada mara moja na magari hayo hurudi barabarani kuchafua mazingira.

“Magari haya yanatumika miaka 10 yanakuja nchini mwetu kutumika tena yanatozwa excise duty mara moja lakini likiingia mitaani linaanza tena kuchafua, tukasema kila mwaka yapewe cheti ya kuonesha yanafanyiwa ukarabati na kuingia tena barabarani,” alisema.

  [caption id="attachment_53195" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mazingira kutoka Jukwaa la Kilimo Tanzania pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ofisini kwake jijini Dodoma leo.[/caption]

Zungu alifafanua kuwa kazi za mfuko wa mazingira zisiwe tu kufanya warsha na mikutano ambayo haigusi uhalisia hivyo maeneo ya mfuko yafanyiwe kazi hasa kwenye uchafuzi wa mazingira, hewa ya ukaa, ukataji wa miti.

[caption id="attachment_53192" align="aligncenter" width="750"] Wadau wa mazingira kutoka Jukwaa la Kilimo Tanzania pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu ofisini kwake jijini Dodoma leo.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi