Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Zungu Afanya Ziara Kiwanda cha Ocean Alluminium
Jun 18, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53371" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Azzan Zungu (Kulia) akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha Ocean Alluminium,Dar es Salaam.[/caption]

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa Azzan Zungu ametembelea kiwanda cha Ocean Alluminium kilichopo Tabata – Matumbi kinachozalisha Sufuria ili kujionea uendeshwaji wa kiwanda hicho pamoja na kutatua changamoto zinazokabili kiwanda hicho ikiwemo kukwama kwa malighafi za Kiwanda hicho katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mhe. Zungu akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt.Samuel Gwamaka pamoja na wataalam mbalimbali wa Serikali, amesema kuwa atakapofanya maamuzi ukaguzi wote stahiki utafanyika.

“Vyombo vya ukaguzi tunavyo na pale tutakapofanya maamuzi hiki wanachokihitaji wamiliki wa kiwanda hiki juu ya mzigo wao huu wa tani 40 hautatoka mpaka wataalam wetu kutoka NEMC pamoja na wataalam wa mionzi kujiridhisha mzigo huu utakuwa ni salama.” Amesema Mhe. Zungu

  [caption id="attachment_53372" align="aligncenter" width="750"] Mhe. Zungu akiwasikiliza viongozi wa Kiwanda cha Ocean Alluminium akiwa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka (Kulia) wakiwasikiliza viongozi wa Kiwanda cha Ocean Alluminium wakati alipofanya ziara kiwandani hapo. [/caption]

Akieleza  kilichowapata hadi shehena yao kuzuiliwa Bandarini Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Arman Arya amesema kuwa waliingiza mzigo huo nchini bila ya kufahamu utaratibu unaopaswa kufuatwa.

“Tuliingiza Kontena la malighafi bila ya kufuata taratibu za hapa nchini. Tulikuwa hatufahamu juu ya taratibu hizo”. Amesema Arya, huku akiongeza kuwa baada ya mzigo wao kuingia nchini ndipo walipofahamu juu ya taratibu hizo na wanamuomba Waziri kama ikiwezekana awasaidie waupate mzigo wao uliokwama Bandarini.

Kutokana na kupokea maombi ya Kiwanda hicho juu ya kupatiwa msaada kutokana na shehena yao ya malighafi kukwama Bandarini, Mhe. Zungu amesema kuwa atashirikiana na vyombo husika kulipatia ufumbuzi suala hilo.

“Tunachukua malalamiko haya ambayo wameyaleta kwangu rasmi maana kwa mujibu wa sheria za Nchi ni Waziri ndiyo mwenye mamlaka ya kushughulikia matatizo na kuhakikisha kama kuna uvunjwaji wa sheria kitu gani kifanywe.” Amesema Mhe. Zungu, huku akiongeza kuwa atashirikiana na Mkurugenzi wa NEMC, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Wanasheria  wa Serikali kutizama namna tatizo hilo linaweza kutatuliwa.

[caption id="attachment_53373" align="aligncenter" width="750"] Waziri Zungu akikagua bidhaa za Sufuria zinazozalishwa na kiwanda cha Ocean Alluminium wakati alipofanya ziara kiwandani hapo.[/caption]

Kwa upande wake Aisha Omary, Meneja Uajiri katika kiwanda hicho anasema kuwa uzalishaji umepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na kukwama kwa malighafi za kiwanda hicho.

“Kiukweli uzalishaji uko chini kutokana na kutokupatikana kwa malighafi lakini tutakapopata malighali za kutosha tunatarajia tutazalisha kwa wingi.” Amesema Aisha

Kiwanda cha Ocean Alluminium Ltd kinazalisha bidhaa za sufuria na soko lake kubwa ni katika masoko ya Jiji la Dar es salaam huku kikiwa na wafanyakazi takriban 100 na kinalipa kodi Serikalini kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2 kwa mwaka.

      [caption id="attachment_53374" align="aligncenter" width="750"] Waziri Zungu akikagua baadhi ya nyaraka mbalimbali za kimazingira za kiwanda cha Ocean Alluminium alipofika katika kiwanda hicho. Picha na Charles Kombe[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi