Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri wa Sheria wa Israel Atembelea JKCI
Apr 25, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30895" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Aleyet Shaked akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi jana ya kuona ushirikiano uliopo wa matibabu ya moyo kwa watoto kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.[/caption] [caption id="attachment_30896" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Aleyet Shaked akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi jana katika Taasisi hiyo. Mhe. Shaked alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo wa matibabu ya moyo kwa watoto, kusomesha madaktari na wauguzi kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel.[/caption] [caption id="attachment_30897" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Aleyet Shaked akiangalia makala ya video inayoonyesha matibabu ya moyo kwa watoto yanayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel. Tangu mwaka 2015 JKCI kwa kushirikiana na SACH ya nchini Israel wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto ambapo watoto wanaokutwa na matatizo wanatibiwa hapa nchini na wanaokutwa na matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu wanatibiwa nchini humo bila malipo.[/caption] [caption id="attachment_30898" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Aleyet Shaked akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo wa matibabu ya moyo kwa watoto, kusomesha madaktari na wauguzi kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi.[/caption] [caption id="attachment_30899" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Aleyet Shaked alipotembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo wa matibabu ya moyo kwa watoto, kusomesha madaktari na wauguzi kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel. Picha na JKCI[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi