Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri wa Nishati ashiriki Mkutano Afrika Kusini.
May 03, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_31134" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa nne kushoto) akiwa akiwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum unaofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya.[/caption] [caption id="attachment_31136" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum unaofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.[/caption]

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameshiriki Mkutano  wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini  ambao pamoja na masuala mengine utajadili suala la uwekezaji katika Sekta ya Nishati.

Katika Mkutano huo unaofanyika tarehe 3-4, Mei, 2018, Dkt Kalemani  ameambatana na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Mhandisi Stella Manyanya na maafisa kutoka Sekta mbalimbali nchini.

Katika Mkutano huo, kampuni mbalimbali kutoka nchini Japan  zimeonesha nia ya kuwekeza nchini katika viwanda mbalimbali ikiwemo vya kutengeneza magari aina ya Toyota.

Mkutano huo umehudhuriwa na kampuni kubwa zaidi ya 200 kutoka nchini Japan, ambapo kampuni hizo zitaonesha teknolojia za kisasa zinazotumika katika kutengeneza vifaa mbalimbali vya kielektroniki na mitambo ya kuzalisha umeme.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi