[caption id="attachment_6532" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi (pichani) akiongea na Watendaji wa Mahakama pindi alipotembelea Mahakama ya Rufani (T) mapema leo na kuonana na Kaimu Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama,Prof. Kabudi amehaidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Mahakama katika utekelezaji wake wa jukumu la utoaji haki nchini, katikati ni Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.[/caption]
Na Lydia Churi-Mahakama
Mahakama ya Tanzania inayo nafasi kubwa katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha inamaliza kwa wakati kesi hasa zile zinazohusu masuala ya kodi ili kuharakisha maendeleo ya nchi.
Akizungumza leo alipotembelea Mahakama ya Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ameitaka Mahakama kuimarisha uadilifu na uwajibikaji ili wananchi wapate haki zao kwa wakati.
[caption id="attachment_6535" align="aligncenter" width="750"]Aidha, Prof. Kabudi alisema anatambua na kuipongeza Mahakama kwa kupanga mikakati ya kuziondosha mahakamani kesi zote za muda mrefu pamoja na kusogeza huduma kwa wananchi kwa kujenga na kukarabati baaadhi ya majengo Mahakama.
Akizungumzia suala la rushwa ndani ya Mahakama, Prof. Kabudi amewataka viongozi wa mahakama kushughulikia suala hilo bila uwoga wala upendeleo.
Wakati huo huo, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma amesema Mahakama itaendelea kushirikiana kwa karibu na mihimili mingine ya nchi ili kuharakisha maendeleo ya nchi.
[caption id="attachment_6537" align="aligncenter" width="750"]Akizungumzia kuhusu sheria, Prof. Juma alisema falsafa ya ni kwa namna gani sheria zinufaishe uchumi wa watanzania ni muhimu kwa kuwa sheria zina mchango katika wa uchumi wa nchi na zinasaidia katika kuondoa umaskini.
Kaimu Jaji Mkuu pia alimshauri Waziri wa katiba na Sheria kutumia Sheria kuinua watanzania wengi hasa wale wenye hali duni za maisha kwa kuwa sheria hutumika katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.
[caption id="attachment_6544" align="aligncenter" width="750"]Naye Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali alisema Mahakama ya Tanzania imefanikiwa katika utendaji kazi wake kwa kuwa hivi sasa asilimia 72 ya mashauri yaliyofunguliwa kwenye mahakama mbalimbali nchini pamoja na yale muda mrefu yamemalizika.
Alisema Mahakama imekuwa ikiyamaliza kwa haraka mashauri yote yanayohusu miradi mikubwa licha ya idadi ndogo ya Majaji waliopo.